TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, November 2, 2014

IGP MSTAAFU PHILEMONI MGAYA ASHEREHEKEA MIAKA 85 YA KUZALIWA KWAKE HUKU WAZIRI MKUU MSTAAFU MSUYA AKIWAASA WATANZANIA.

WAZIRI Mkuu
Mstaafu Cleopa Msuya amewaomba watanzania
kuwa na tabia ya utii wa sheria, uaminifu na uadilifu katika nafasi zao
wanazozitumukia katika Taifa la Tanzania.
Msuya aliyasema hayo katika sherehe ye kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya iliyofanyika katika Hotel ya Protea , Court Yard jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu alieleza kuwa tabia aliyoionyesha Mgaya wakati wa utumishi wake serikalini inapaswa kuigwa na watanzania wote.
“Huyu ndiye Mtanzania halisi aliyelelewa vizuri kuitumikia nchi yake. Hana makuu, ni mkweli
na mwadilifu. Akiahidi kufanya jambo fulani analitekeleza bila kuchelewa.
Tunahitaji uwajibikaji wa namna hii,” Msuya alisisitiza.
Alisema kuwa Mgaya alikuwa kiongozi hodari ambaye alisimamia vyema kiapo na kazi zake na kipindi chake cha uongozi  alikuwa akitoa amri zinatekelezwa mara moja.
Naye Mshauri wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited James Rugemalira alitoa wito kwa watanzania kuendele kuunga mkono  jitihada za kuendeleza maeneo mbalimbali ya kiuchumi ikiwemo viwanda.
Aliwasihi wadau kutoa ushirikiano kwa  kampuni yake inayosambaza
bia aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught ambayo inadhamira ya kujenga kiwanda cha kuzalisha bia hizo hapa nchini.
                                       
“Tunatafutamaeneo Kilimanjaro, Tanga na Bukoba ili tuweze kujenga kiwanda hapa nchini.
Tumedhamilia kufanya hivyo na tutafanya,” Rugemalira alisisitiza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira aliwashukuru wananchi kwa kukubali kujumuika pamoja katika hafla hiyo na kumwomba Mzee Mgaya aendelee kuwapa mwongozo wa namna ya kuenenda katika maisha.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa aliwaomba watanzania kuwa na moyo wa unyenyekevu na kujitolea kulitumikia taifa katika utumishi wao kama ilivyokuwa kwa IGP mstaaafu Mzee Mgaya.
Wageni wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara, Katibu Mkuu Msaaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Bakari Mwapachu, Balozi Antoni Nyaki na wazee wengine maarufu kama Timothy Msangi.
 Mara Baada ya Ibada katika Kanisa la Azania Front wakati wa  kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya
Baadhi ya waumini mbalimbali wakiwa nje baada ya Ibada
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Mstaafu Philemoni Mgaya akiwa katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
 Keki
Waziri  Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimpongeza aliyekuwa IGP Philemoni Mgaya
 Mzee Timothy Msangi akieleza Historia fupi ya IGP Mstaafu Philemoni Msangi
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu

No comments:

Post a Comment