TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, November 3, 2014

CHETI CHA WILAYA WANGINGOMBE CHAKABIDHIWA NA RC NJOMBE

 
Na James Festo, Wangin'gombe.

MKUU wa mkoa wa Njombe hapo juzi amekadhidhi cheti kwa Halmashauri ya Wilaya Wanging'ombe kinachoonyesha makao makuu ya Wilaya hiyo ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo cheti ambacho kimetoa kauli ya serikali itakayoondoa utata wa makao makuu.

Awali cheti hicho kilikosewa katika uchapaji wa eneo maalumu la kujengwa kwa makao makuu, ambapo kilionyesha  makao makuu yalitakiwa kuwepo Wanging'ombe  badala ya Igwachanya yaliposasa na kusababisha kuibuka tena kwa mvutano juu ya sehemu sahihi  ya makao makuu ya wilaya hiyo licha ya kutangazwa na serikali.

Akizungumza katika Makabidhiano ya Cheti hicho yaliyofanyika katika baraza la madiwani wa halmashauri hiyo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi  aliwataka watendaji wa halmashauri hiyo kupanga mipango yake vema kwani cheti wameshakipata ambacho kinaonyesha uhalali wa wilaya hiyo na kuacha malumbano ya kisiasa.

" kuna waliotaka iwe wangin'gombe  wengine iwe igwachanya na wengine walitaka iwe Mdandu, lakini mwenye uamuzi wa mwisho ni Rasi kwa mujibu wa sheria kwenye gazeti la serikali la mwezi april mwaka jana  ilitangaza kuanzishwa kwa halmashauri 19 ikiwemo hii ya kwenu" alisema Msangi

"Kwa bahati mbaya spika wa bunge alikosea kuandika jina la makao makuu itakuwa wangin'gommbe imetuchukua mda mrefu kufuatilia lakini hatimaye tumefanikiwa na leo nimekuja rasmi kuwakabidhi cheti chenu" aliongeza Mkuu wa Mkoa.

Aidha Msangi aliwataka viongozi hao kuitumia fursa hiyo kama chachu ya kufanya maendeleo  ikiwemo kuweka mji huo katika mpango mzuri wa majengo kwani endapo wakifanya kosa katika hilo itasababisha kutokuwepo kwa muonekano mzuri wa mji.

"kazi ni kwako mtu wa mipango miji tusifanye kosa kama walivyofanya wenzetu kwenye miji mingine hapa nchini, tufanye kitu ambacho kitakuwa tunu kwa wananchi ambao watakuja kuishi miaka mingi ijayo" alisema Msangi.

Kwa Upande wake Kamanda wa Tume ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Njombe Bw. Charles Nakembetwa  aliwataka watumishi wa halmashauri hiyo kuongeza bidii katika shughuli za maendeleo bila ya kuhusiha masuala ya rushwa.

"nyinyi ni wapya mkifanya kosa leo kitakuwa ni kilio cha halmashauri milele na milele..wewe kama mtumishi unaweza kusema unapita tu sawa lakini hata wewe unandugu zako watanzania ambao watakuja kutumia majengo, barabara hizo hizo ulizoamua kujenga chini ya kiwango
kwa sababu ya tamaa yako" alisema Nakembetwa.

Naye Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Bw. Antony Mahwata alimuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa  wataendelea kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na kuishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa kwa juhudi walizozifanya hadi kupatikana kwa cheti hicho.

"kwa niaba  ya wenzangu tunashukuru serikali ikishasema hilo ni agizo tunatakiwa kulitekeleza  tutahakikisha kila kitu kinajengwa kwa kiwango  kinachotakiwa na tunashukuru pia kupata cheti ambacho kinaonyesha uhalali wa Halmashauri yetu"alisema Mahwata.

Aidha katika bejeti ya mwaka 2014/2015 jumla ya shilingi milioni 14 zilitegwa kwa ajili ya upimaji wa viwanja katika eneo la Mjini  Igwachanya wilaya ambayo inatoka katika wilaya mama ya Njombe na ina jumla ya Kata 17.

No comments:

Post a Comment