TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, November 2, 2014

Taarifa ya tukio lililotokea ubungo plaza katika mkutano wa mwalimu Nyerere foundation

IMG-20141102-WA0021
 Mkutano ulifanyika kuanzia saa 1520hrs ukiwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu mh. Joseph Sinde Warioba. Mkutano ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na itikadi tofauti za kisiasa. Mkutano ulirushwa moja kwa moja na ITV na maudhui yake kimtazamo ulilenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya tume ya Warioba na ile ya Mh. Sitta na tume yake. Baada ya Mh. Warioba kuelezea kwamba Muungano sio tunu ila ni urithi ndipo wakereketwa wa upande wa Mh. Sitta walipoinua mabango yasemayo pamoja na mambo mengine kwamba iweje wajadili mapendekezo ya katiba ya Mh. Sitta ambayo wao wameshaikubali? Baada ya mabango yale kuinuliwa yakazua tafrani ambapo walishauriwa kutoyainua kwa sababu haukuwa mkutano wa kisiasa na wakanyang’anywa na kuyachana ndipo vurugu/kashfa/matusi yakaanza kutolewa dhidi ya meza kuu. Hali hii ilisababisha kushikana, kusukumana na kurushiana viti. Katika tafrani hiyo mh. Warioba alipigwa kibao na Mh. Paulo Makonda- ambaye ni katibu wa UVCCM TAIFA. Mtuhumiwa huyu pamoja na wengine wanne wamekamatwa kwa mahojiano. Upelelezi unaendelea na juhudi za kuwapata wengine zinaendelea.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Kidata atembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu NHC Mkinga

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Japan Kidata akisikiliza maelezo ya Meneja wa miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Gugadi huku Kaimu Mwenyekiti wa  Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa na Mkurugenzi wa Fedha, Felix Maagi akisikiliza, kulia kabisa ni Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera, Ng’aranga Magai. Katibu Mkuu Kidata alitembelea mradi huo leo hii ili kuweza kufahamu utendaji wa NHC katika miradi ya nyumba ya gharama nafuu, jana alifungua kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Japan Kidata akisikiliza maelezo ya Meneja wa miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Gugadi huku Kaimu Mwenyekiti wa  Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa na Mkurugenzi wa Fedha, Felix Maagi akisikiliza, kulia kabisa ni Meneja wa NHC Mkoa wa Kagera, Ng’aranga Magai.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Japan Kidata akifutilia maelezo ya Kaimu Mwenyekiti wa  Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa na Mkurugenzi wa Fedha, Felix Maagi katikati yao ni Meneja wa NHC Mkoa wa Upanga, Nathaniel Malisa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Alphayo Japan Kidata akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utawala wa Mikoa wa Shirika la Nyumba la Taifa, Raymond Mndolwa, kushoto ni Meneja wa NHC Mkoa wa Dodoma, Itandula Gambalagi
Baadhi ya nyumba zilizokamilika zinavyoonekana
Sabina Kilato wa NHC Kigoma akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Margareth Ezekiel, Kaimu Mkuu wa Mkadiriaji Majengo wa NHC wakati wa ziara hiyo iliyowashirikisha Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Mameneja na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa. 
Baadhi ya Wajumbe waliokuwapo katika ziara hiyo
Baadhi ya nyumba zilizokamilika zinavyoonekana.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio akijadiliana jambo na Meneja wa NHC mkoa wa Tanga, Isaya Mshamba na Meneja wa Rasilimali watu wa NHC, Omari Makalamangi wakati wa ziara hiyo iliyowashirikisha Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Mameneja na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio akijadiliana jambo na Meneja wa NHC mkoa wa Tanga, Isaya Mshamba na Meneja wa Rasilimali watu wa NHC, Omari Makalamangi wakati wa ziara hiyo iliyowashirikisha Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Mameneja na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki, Hamad Abdallah.
Meneja wa miradi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Subira Gugadi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Ubunifu, Issack Peter. Katikati ni Mohammed Mneka, Katibu wa TAMICO NHC.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Mameneja na Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa waliofika katika ziara hiyo.
Baadhi ya nyumba zilizokamilika zinavyoonekana.
Baadhi ya nyumba zilizokamilika zinavyoonekana.

No comments:

Post a Comment