TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, November 3, 2014

Serikali haipo tayari kuona Karafuu ya Zanzibar inapoteza hadhi na ubora wake

D92A1837
Na Ali Mohamed Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Juma Ali Juma amesema serikali haipo tayari kuona Karafuu ya Zanzibar inapoteza hadhi na ubora wake wa asili kutokana na kuchafuliwa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu. Akizungumza katika semina ya ubora wa zao la karafuu kwa maendeleo ya Zanzibar katika Ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Pemba alisema hatua zitachukuliwa kudhibiti hali hiyo. Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo malalamiko ya wateja na matukio ya kupungua uzito wa karafuu zinazosafirishwa nje ya nchi ambapo sababu hizo zinasababishwa na karafuu kutokauka vizuri na kuchanganywa na vitu visivyohitajika. Alisema Wakaguzi na wapasishaji katika vituo vya manunuzi ndio dhamana na wanawajibika kisheria juu ya kulinda ubora wa karafuu hivyo hawatakiwi kupasisha karafuu zisizokuwa na ubora unaotakiwa. Alisema kuwa kutakuwa na utaratibu wa kufatilia karafuu zinazonunuliwa vituoni ili kuwajua wapasishaji wanaozembea ama kula njama katika kutekeleza wajibu huo na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakao bainika. Nae Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar ZSTC Mwanahija Almas Ali alisema Shirika limeingiza mashine ya kupima ubora wa karafuu kwa majaribio na endapo ikifaa zitawekwa katika vituo vyote vya manunuzi. Alisema dhamira ya Shirika ni kusafirisha karafuu zenye ubora maalumu na kusisitiza kuwa ni lazima yawepo mashirikiano kati ya wadau wote wa zao la karafuu juu ya kulinda ubora unaotakiwa. Akiwasilisha mada ya ubora wa karafuu Mkurugenzi Masoko wa ZSTC Abdlla Salum Kibe alisema karafuu bora zinatakiwa ziwe safi, zimekauka vizuri, ziwe na rangi ya dhahabu na zilizoanikwa kwa kutumia jua. Alizitaja sifa nyengine kuwa ni Karafuu zisizochanganywa na aina yo yote ya taka, zilizoanikwa kwa mpangilio unaokubalika wenye kupitisha hewa na zenye unyevu wa kiwango kinachokubalika cha 14%. Kwa upande wao Wakaguzi na Wapasishaji wamesikitishwa na matukio hayo ya kununuliwa karafuu chini ya kiwango cha ubora na kudai kuwa wao wanajitahidi kwa kila hali kutekeleza kazi zao kwa uadilifu. Aidha waliahidi kuwa wataendelea kuwa waadilifu na makini zaidi katika utendaji kazi na waliiomba serikali kuendelea kuwapatia mafunzu maalumu na vifaa vya kisasa ili kuongeza ufanisi wa kazi hiyo muhimu.

No comments:

Post a Comment