TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, November 3, 2014

MAELFU WAJITOKEZA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA- MDEE AFUNIKA SHINYANGA- AMFUNIKA MAGUFULI,



Maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga na maeneo ya jirani waliojitokeza jioni ya jana katika viwanja vya mahakama ya mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga katika mkutano mkubwa wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa ndugu Halima Mdee ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kawe.Pamoja na mambo mengine viongozi mbalimbali wa Chama hicho walisisitiza umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa Desemba 14,2014 huku wananchi wakishauriwa kuachana na propaganda za CCM ambayo imeshindwa kuwaondoa Watanzania katika umaskini,kila siku maisha yanazidi kuwa magumu
 (Picha Zote na Kadama Malunde-Shinyanga)
Viongozi mbalimbali wa Chadema ngazi ya wilaya,mkoa na taifa wakiwa jukwaa kuu jioni ya leo mjini Shinyanga
Mbunge wa Kawe kwa tiketi ya Chadema akiongea na wakazi wa Chato mkoani Geita hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), Halima Mdee, amebomoa ngome ya mbunge wa Chato, Dk. John Magufuli kwa kuzoa wanachama zaidi ya 300 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwa katika ziara yake wilayani Chato, Mkoa wa Geita.
Dk. Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, amejizolea umaarufu mkubwa nchini kiasi cha kujijengea taswira kwamba anaungwa mkono jimboni kwake, ambapo sasa kwa pigo hilo la Mdee, atapaswa kujipanga upya.
Akiendelea na ziara yake ya Kanda ya Ziwa ya kuimarisha chama na kuhamasisha wananchi waikatae Katiba mpya inayopendekezwa, Mdee  aliwapokea wanachama hao wa CCM na kuwakabidhi kadi za CHADEMA kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya zamani.
Wanachama hao walieleza kuwa sababu iliyowasukuma kukihama chama hicho ni kutokana na kuchoshwa na kauli za kejeli za mbunge wao, Dk. Magufuli kila wanapomhoji kuhusu utekelezaji wa ahadi zake.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Christopha Masanja alisema kuwa wanakabiliwa na kero nyingi ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama licha ya kuwa karibu na ziwa Victoria, lakini kila wanapojaribu kumweleza mbunge wao, huishia kuwapa kauli za kejeli.
Akihutubia umati mkubwa wa wananchi, Mdee alisema kuwa serikali ya CCM imekuwa haiwathamini wananchi wake ndio maana imeshindwa kutoa kipaumbele kinachostahili katika kutatua kero zao na badala yake kuelekaza fedha nyingi kwenye mambo yasiyo na msingi.
Alisema kuwa sekta ya kilimo inayotoa ajira kwa Watanzania zaidi ya aslimia 80 imetengewa kiasi kidogo cha fedha kwenye bajeti ya mwaka huu
ya sh. bilioni 42  huku safari za rais zikitengewa sh. bilioni 50.
Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe, aliwataka wananchi wa Chato kufanya mabadiliko na kuondoa uteja kwa CCM akisema kuwa licha ya kuwapa kura tokea nchi ipate uhuru lakini wameshindwa kuwatatulia kero zao.
Aliwataka kutorudia makosa hayo kwenye chaguzi zijazo badala yake wahakikishe kwenye ngazi zote za uwakilishi wanachagua wagombea watakaosimamishwa na CHADEMA.
Chanzo: Tanzania Daima.

No comments:

Post a Comment