TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, November 3, 2014

TAMASHA LA UPENDO KWA MAMA KURUDIWA MWISHONI MWA MWEZI HUU

sam_0675
Mahmoud Ahmad Arusha
Tamasha la upendo kwa mama lilofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kushindwa kumalizika sababu ya mvua linatarajiwa kurudiwa mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza kabla ya kuahirishwa kwa Tamasha hilo mratibu wa tamasha hilo Carlos Mkundi alisema kuwa tamasha hilo litarudiwa na hakutakuwa na kiingilio tarehe 30 ya mwezi huu huku akiwataka kuwa na moyo wa uvumilivu kwani kila jambo linahitaji uwepo wa bwana.
Hata hivyo kabla ya wasanii Christina Shusho na Upendo Nkone kupanda jukwaani mvua kubwa ilianza kunyesha hivyo kukatiza kiu ya wauumini mbalimbali waliojitokeza kupata burudani ya nyimbo za injili iliyokuwa itolewe na wasanii hao.
Iliwabidi  waimbaji maarufu wa nyimbo za injili waliokuwa wakijiandaa kupanda jukwaani ndipo mvua kubwa iliyoambatana na upepo ilianza kunyesha hali iliyowafanya wasanii hao kuimba bila ya kutumia vyombo na kipaza sauti huku washiriki wakiimba pamoja nao na baadae kuahirishwa kwa tamasha hilo.
Awali kabla ya wasanii hao kuwasili katika uwanja huo makundi mbali mbali yaliwapa burudani waumini mbali mbali waliofika katika uwanja huo wakisubiri kuona burudani kutoka kwa wasanii nguli wa nyimbo za injili akiwemo Martha mwaipaja,Christina Shusho,Carlos Mkundi,Matumaini, na Upendo Nkone.
Hakika tamasha hilo lilijaa furaha kwa waumini na wakazi mbal;I mbali wa jiji la Arusha kujitokeza kwa mamia kujakushuhudia burudani hiyo huku wakiimba na kucheza muziki wa kumtukuza mungu kwa furaha.
Ndipo katika hali isiyo ya kawaida mvua ilianza kunyesha majira ya saa 11 jioni na kukatiza burudani hiyo huku wakazi hao wa jiji la Arusha kulazimika kukimbilia jukwaa kuu kujificha mvua hvyo tamasha kuahirishwa hadi mwishini mwa mwezi huu.

No comments:

Post a Comment