TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, November 3, 2014

OLX YAJIAANDAA KUINGIA TANZANIA

Olx
Uongozi waeleza ushirikiano na Facebook ni hatua ya kwanza
OLX, moja ya jukwaa linaloongoza majukwaa yatoayo habari kwa njia ya mitandao Duniani leo limetangaza kuingia kwenye soko la Tanzania kwa kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Bw. Thomas Plateng
a, kiongozi wa OLX Kusini mwa Jangwa la Sahara ameelezea furaha ya kampuni yake kuaza mradi huo. “OLX imekuwa na mafanikio makubwa kwenye nchi ambazo inapatikana. Kenya tumefanikiwa kuwaelemisha watu kuhusu ya mtandao wetu kwa asilimia 98 (98%). Hii ina maana kuwa kila mtu anaijua OLX na anaweza kukuambia inahusika na vitu gani. Tuna tumaini tutapata muamko wa aina hii kutoka Tanzania,” alisema Bw. Platenga.
Takwimu zinaonyesha kuwa, inakadiriwa ni asilimia 4.4 (4.4%) ya Watanzania wanapata huduma ya mtandao (internet) huku Facebook ikiwa ni moja ya huduma inayotumiwa zaidi. Hii inaashiria kuwa ni fursa ya kuwaunganisha watu wengi na OLX.
“Ushirikiano wa baina ya Facebook na OLX ni muhimu sana kwetu. Mtandao wetu una mambo mengi ya kutoa, na tunaamini kwa kutumia njia na taarifa sahihi tutafanya mapinduzi ya biashara ya mtandaoni Barani Afrika,’’ aliongeza Bw. Platenga. 
OLX inapatikana kwenye nchi zaidi ya 100 Duniani na inatumia lugha 50 tofauti. Hii inasaidia kutafsiri lugha kwa mamilioni ya watu Ulimwenguni kote kila siku wanaotumia OLX kununua na kuuza bidhaa, kutafuta kazi au kupangisha nyumba. Zaidi ya watumiaji tofauti milioni 200 kwa mwezi wanatimiza jumla ya wasomaji wa ukurasa wa OLX zaidi ya bilioni 11 kwa mwezi au wasomaji wasiopungua milioni 360 kwa siku hivyo OLX ina matumaini ya kuzidi kukua na kupanua huduma zake Afrika.
Bw. Platenga alihitimisha kwa kusema kuwa kuingia Tanzania ilikuwa ni moja ya mkakati muhimu. “Tovuti yetu Tanzania imeshaanza kufanya kazi na sasa kupitia ushirikiano na Facebook hasa ukizingatia OLX ni moja ya huduma za bure ndani ya huduma za mtandaoni hivyo Watanzania watafanya biashara,” alisisitiza Platenga
Huduma ya Facebook inafanya matumizi ya mtandao kuwa rahisi kupitia huduma za bure ambazo zinawawezesha watu kuperuzi mambo mbalambali kwenye tovuti bila kulipia.
Wateja wa mtandao wa tigo nchini Tanzania wanaweza kupata huduma ya internet kupita Google Play kwa kutembelea tuvuti ya www.internet.org kwa kutumia simu ya mkononi kupitia Opera Mini. Huduma hii inapatikana kwa watumiaji wa smart phones na simu za kawaida zenye uwezo wa internet.
Kampuni ya OLX ina wafanyakazi 600  kwenye ofisi zake zilizoko Buenos Aires, Cape Town, Delhi, Sao Paulo, Rio de Janeiro, Lisbon, New York na Kenya.

No comments:

Post a Comment