TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, November 3, 2014

HOSPITALI YA KAIRUKI YAPATA TUZO

unnamed
Mkurugenzi mkuu wa hospital ya Kairuki, Dkt Asser Mchomvu (kulia) akiwa amebeba tuzo aliyokabidhiwa na na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto). Picha na mpigapicha wetu.
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ameukabidhi uongozi wa Hospitali ya Kairuki (KH) tuzo ya waliofanya vizuri katika vigezo mbalimbali vya uboreshaji viwango vya huduma ya Afya katika mkutano wa 4 wa kitaifa kuhusu uboreshaji Viwango vya huduma ya Afya uliofanyika wiki iliyopita (Octoba 31-2014) katika ukumbi wa mikutano wa Benki kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.
Akizungumza na gazeti hili jana, Naibu MKurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Muganyizi Kairuki alisema sifa ya mafanikio yao mpaka wakapata tuzo hiyo yanatokana na mafunzo kwa wafanyakazi wa Hospital wapatao 20 yaliyoendeshwa na Wizara ya afya ikishirikiana na Jhpiego,CDC na PEPFAR.
Dkt. Kairuki aliongeza kuwa ni mafunzo kuendelea kutolewa na wakufunzi wa ndani ( inhouse training), kuundwa kwa timu maalum ya ndani kwa ajili kufanya ukaguzi wa kushtukiza ndani na utayari wa KH kushirikia katika zoezi la udhibiti na uzuiaji wa maambukizi.
Aidha, Dkt. Kairuki alieleza kuwa siri nyingine ni ushirikiano mzuri baina ya manegimenti ya KH na timu ya wakaguzi toka wizara ya Afya katika kutekeleza maagizo na mapendekezo na kuyafanyia kazi.
“Kwa upande wetu maeneo yaliyofanya vizuri katika zoezi ili ni pamoja na mashine bora za kuuwa vijidudu (sterilization unit) na eneo zima katika kitengo hicho, eneo la kuifadhi/ kutenganisha na usafirishaji wa taka hatarishi, taka mbichi na taka mchanganyiko pia chumba cha upasuaji kufuata taratibu stahiki za kimataifa katika kuzithibiti maambukizi,” alisema Dk Kairuki
Aliongeza kuwa wakati huohuo KH imezindua kampeni maalum za muda mrefu katika kuchunguza na kutibu magonjwa yasiyoambukiza, mfano saratani ya matiti, saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya tezi dume (prostate). Saratani hizi ndizo zinazoongoza kwa hapa nchini.
“Lakini pia KH imezidi kuboresha huduma katika vitengo vya macho, sikio, pua na koo kwa kupata mitambo ya kisasa katika nyanja hizo,” alisema Dk Kairuki
Aliongeza kwakusema kuwa KH imezindua wodi mpya ya kisasa hasa kwajili ya wanachama wa mfuko wa Bima ya taifa ya afya.(NHIF) na wodi maalum ya watoto.
Wengine waliotunukiwa tuzo hizo za uboreshaji wa huduma za afya ni Hospitali ya Bugando-Mwanza pamoja na Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC). Tuzo hizo zilitolewa na Wizara ya Afya wakishirikiana na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Marekani (CDC) na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR).

No comments:

Post a Comment