TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, September 30, 2014

SAKATA LA MAKABURI LACHUKUWA SURA MPYA.

Mahmoud Ahmad Arusha
Sakata la kuhamisha makaburi lachukuwa sura mpya baada ya KAMATI ya kusimamia makaburi ya waislamu yaliyopo eneo la Levolosi jijini Arusha, kusisitiza kuwa haijafanya mazungumzo yeyote na halmashauri ya jiji la Arusha, kuhusu kufukuliwa kwa makaburi hayo yaliyopo eneo la Levolosi na badala yake kujengwa kituo kikubwa cha mabasi madogo yanayotoa huduma zake jijini Arusha na maeneo ya jirani, Daladala.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ustaadhi Omari Bokolo, akizungumza kwenye eneo la makaburi hayo amesema eneo hilo halijabadilishwa matumizi  na wala hawana mpango huo wa kubadili matumizi ya eneo hilo kwa sasa  .
Amesema kuwa eneo hilo la makaburi sio mali ya halmashauri ya jiji la Arusha kama ilivyodaiwa.bali eneo hilo linamilikiwa mtu binafsi ambae ni marehemu Said Sela Said tangia mwaka 1940, ambae kabla hajafariki aloilitoa wakfu kwa waislamu watakaokuwa wakifariki jijini Arusha  kuzikwa hapo .
Ustaadhi Bokolo, amesema kamati hiyo ya kusimamia makaburi ya waislamu katika jiji la Arusha, imeshutushwa na tamko la mkurugenzi wa jiji la Arusha Idd Juma, alilolitoa mwishoni mwa wiki kuwa tayari ameshazungumza na viongozi wa kiislamu na kukubaliana eneo hilo kubadilishwa matumizi kutoka makaburi na kujengwa  kituo cha daladala.
Amesema kamati inazo nyaraka zote za tangia mwaka 1940 hadi leo na kuutaka uongozi wa halmashauri ya jiji kurejea kwenye kumbu kumbu ili kuelewa umiliki halali wa eneo hilo .Amesema kuwa mwaka 2006 baada ya kutokea mgogoro wa  umiliki kutokana na mbinu chafu zilizofanywa na baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya madiwani, kamati hiyo ilimwandikia waziri wa Ardhi wakati huo, Dakta John Magufuli, ambae alithibitisha kuwa eneo hilo haikuwa mali ya halmashauri ya manispaa ya Arusha kwa wakati huo na kuitaka kamati hiyo kuliendeleza .
Ameongeza kuwa mwaka 2013 waziri wa Ardhi ,Profesa Anna Tibaijuka, katika mlolongo huo aliiagiza halmashauri ya jiji la Arusha kukaa  na kamati hiyo kutatua mgogoro huo lakini hilo halijawahi kufanyika  na badala yake halmashauri ya jiji inatangaza kubadilisha matumizi ya eneo hilo.
Wajumbe wa kamati hiyo wamehoji  uhalali wa halmashauri kumiliki eneo hilo sanjari na kushangazwa na hatua ya kutaka kujenga kituo cha daladala kati kati ya jiji badala ya huduma hiyo kujengwa maeneo ya pembezoni ambayo hayana msongamano na wakaitaka halmashauri kusitisha mara moja mpango huo vinginevyo wataiburuza mahakamani .
Mwishoni mwa wiki mkurugenzi wa jiji ,Idd Juma, amesema kuwa wanakusudia kubadili matumizi ya eneo hilo kutoka makaburi na kujengwa kituo cha daladala ili kuondoa msongamano  wa daladala katikati ya jiji la Arusha.

No comments:

Post a Comment