Wazee wakiwa kwenye kongamano la
 wazee kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mpanda kujadili 
changamoto zinazowakabili wakati wa kupatiwa matibabu.
Na Kibada  Kibada-Katavi.
Wahudumu wa Afya wameendelea 
kuwanyanyapaa wazee wawapo hospitalini kupata huduma ya Afya kwa 
kuwaacha wakae asubuhi hadi jioni ,huku wenyewe wakifanya kazi zao 
nyingine.
Pia wakitibiwa na Daktari  mara 
nyingi huambiwa wakatafute dawa madukani hata kama zipo hospitalini na 
ukiuliza kwa nini hujibu hawahitaji usumbufu.
Hayo yameelezwa na Katibu wa 
Shirika la Wazee saidia lenye makao yake Wilayani  Kasulu Mkoani 
 Cotlida Kokupima wakati akiwasilisha salamu za wazee kutoka Mkoani 
kigoma kwenye kongamano la wazee lililofanyika Mjini Mpanda Mkoa wa 
Katavi.
Bibi Kokupima ameeleza 
changamoto zinazowakabiliwa wazee katika maeneo mbalimbali zikiwemo na 
manyanyaso hayo wanayofanyiwa wazee wakiwa katika Zahanati,Vituo vya 
Afya Pamoja na Kwenye Hospitali mbalimbali hapa nchini.
Changamoto hizo ni kuwa wakienda
 kutibiwa na wakishaandikiwa dawa wanaambiwa hazipo waende wakanunue 
madukani wakati mwingine wanakuwa hawana hela matokeo yake wanarudi 
nyumbani kulala bila kupata dawa na mwisho ni kufa.
Changamoto ya usafiri kutoka 
nyumba hadi kufika kwenye huduma za jamii hasa matibabu kwa wazee wenye 
umri mkubwa ni taabu,hawana uwezo wa kuzifuata dawa dukani hata kama 
watakuwa na fedha.
Kwa Upande wake mwakilishi wa 
shirika la Afya la Wazee Duniani Athman Daniel ameeleza kuwa shirika 
lake kwa kusaidiana na wadau mbalimbali na wazee limeweza kuchangia 
kuisukuma serikali kuona uwezekano wa kuwapatia wazee malipo ya uzeeni 
na mchakato unaenda vizuri na  wakati wowote suala hilo litafanikiwa.
Akizungumzia Halmashauri ya 
Mpanda amesifu juhudi zilizofanywa  katika kuwahudumia wazee kwa kutenga
 chumba cha kiliniki ya wazee na wanapatiwa huduma hapo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “WAZEE WASIACHWE NYUMA TUJENGE JAMII SHIRIKISHI KUPITISHA  SHERIA YAO.

No comments:
Post a Comment