CRDB
 Microfinance Insurance Brokers ambao ni wakala wa bima za aina zote 
ikiwemo bima ya afya, moto, nyumbani na maisha wakishirikiana na kampuni
 zaidi ya kumi za bima nchini Tanzania,wamefanikiwa kuwapatia huduma ya 
bima ya maisha,mazishi na ulemavu wa kudumu Kundi la Wasanii wa 
Vichekesho  la Orijino Komedy Company wao na familia zao kupitia African
 life Assurance (Tanzania) Ltd na bima ya afya wao na familia zao 
kupitia Kampuni ya AAR Insurance Tanzania.
CRDB 
Microfinance wanayo furaha kubwa kwa kuwapatia wasani hao huduma 
hiyo,kwani siku zote imekuwa ikifahamika kuwa msanii ni kioo cha 
jamii.Wasanii hao waliofanikiwa kujiunga na huduma hizo ni pamoja na 
Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’, Mjuni Silvery ‘Mpoki’, Lucas Mhuvile 
‘Joti’, Alex Chalamila ‘McRegan’  na Kiongozi wa kundi hilo,Sekioni 
David na wengine ni Herry pamoja na Jonas.
Huduma
 hii inawahamasisha wasanii wengine,wanahabari,wanamitindo na watanzania
 wote wa hali zote kutembelea ilipo CRDB Bank tawi lolote nchini 
Tanzania,ili waweze kupata huduma nzuri ya na  haraka ya bima “ndani ya 
mikono salama” .
Meneja
 wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha (kushoto) 
akimkabidhi Kadi ya huduma ya bima ya maisha,mazishi  na ulemavu wa 
kudumu Kiongoni Mkuu wa Orijino Komedy Company,Sekioni David (kulia) 
wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo kwenye ofisi za CRDB Mikocheni 
jijini Dar.
Msanii Lucas Mhuvile ‘Joti’ akipokea kadi yake  kutoka kwa Meneja wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Arthur Mosha.
 Msanii
 Isaya Mwakilasa ‘Wakuvwanga’ (kulia) akipokea kadi yake kutoka 
kwa Meneja wa CRDB Microfinance  Insurance Brokers,Arthur Mosha.(wa pili
 kulia) ni Meneja Mkuu wa African Life Assurance,Nura Masoud na Kushoto 
ni Meneja Mkuu wa AAR Insurance,Majala Manyama.
Meneja
 Uhusiano wa CRDB Microfinance Insurance Brokers,Nargis Mohamed (kulia) 
akiwa na  Msanii wa Kundi la Wasanii wa Vichekesho la Orijino Komedy 
Company,Mjuni Silvery ‘Mpoki’ katika hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment