Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waki wa katika picha ya pamoja kabla ya mtanange dhidi ya RAS Simiyu leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
Waamuzi
 wa mchezo mpira wa miguu kati ya timu ya Wizara ya Habari, Vijana, 
Utamaduni na Michezo na RAS Simiyu wakiongozwa na mwamuzi wa kati 
Ramadhani Omari (wa pili kulia) wote kutoka kituo cha michezo ya vijana 
chini ya miaka 20 kijulikaanacho kama Twalipo cha mjini Morogoro.
Mchezaji
 wa timu ya mpira wa pete Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
 Agnes Mbambo akimiliki mpira wakati wa mechi yao na Wizara ya Ardhi, 
Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenye mashindano ya SHIMIWI leo mjini 
Morogoro.
Wachezaji
 Johari Kachwamba (kulia) na Hadija Omari Jaa (kushoto) wakiwa kwenye 
harakati za kuwania mpira wakati wa mechi kati ya Wizara ya Habari, 
Vijana, Utamaduni na Michezo na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya 
Makazi.
(Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Timu ya Habari SHIMIWI yatoa kipigo kwa RAS Simiyu.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
29/09/2014
Timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
 Michezo imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika 
mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Watumishi wa Wizara na Idara za 
Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mjini Morogoro.
Wakicheza kwa kuonana timu hiyo ikiongozwa na Nahodha wao Carlos
 Mlinda walilisakama lango la wapinzani wao RAS Simiyu ambapo katika 
kipindi cha kwanza mcheza aliyevalia jezi yenye namba 11 Erick Mfugale 
aliwapatia goli la kuongoza kwa kipindi cha kwanza hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilinza kwa timu zote kusaka ushindi ili kujihakikishia hatua inayofuata.
Dakika ya saba ya kipindi cha pili mchezaji aliyevalia jezi 
namba 8 Maurus Ndenda ndiye aliwanyanyua mashabiki wa timu ya Wizara ya 
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kufunga goli la pili kwa shuti 
kali na kuingia wavuni.
Hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi wa mchezo huo Ramadhani 
Omari, timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeshinda 2
 na RAS Simiyu hawajapata kitu ambapo ubao wa matokeo ulisomeka (Habari 
2-Simiyu 0).
Aidha kwa upande wa mpira wa pete timu ya Wizara ya Habari, 
Vijana, Utamaduni na Michezo leo bahati haikuwa yao wamefungwa goli 39 
kwa 10 na wapinzani wao Wizara ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo ya Makazi.
No comments:
Post a Comment