Kaimu
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dr. Asha Mahita akizungumza na wajumbe 
muda mchache  kabla ya Mgeni rasmi kufungua kikao rasmi. Kushoto ni Mkuu
 wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dedengo na kulia Chama cha Watoa Huduma 
binafsi za Afya Nchini, Dr. Samweli Ogillo.
SERIKALI  imetoa rai kwa wananchi 
kutoa taarifa kwa mgonjwa yeyote mwenye  dalili ya ugonjwa wa Ebora ili 
aweze kupati msaada wa kitabibu hali ambayo itapunguza maambuzi kwa watu
 wengi .
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa 
Wilya ya Tanga wakati akifungua kikao cha maelekezo huhusu ugonjwa 
hatari wa Ebola na dhana ya ushirikiano baina ya Sekta binafsi na Sekta 
ya Umma kwa madaktari na wauguzi kutoka serikalini na sekta binafsi 
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Rodasaksa Hospiali ya Mkoa wa Tanga 
(Bombo).
Kikao hicho ni moja ya jitihada 
ambazo zinachukuliwa na Mkoa wa Tanga katika kutoa uelewa  wa ugonjwa 
huo hatari ambao sasa  umekuwa tishio katika baadhi ya maeneo ya Afrika.
  Vile vile ametoa wito kwa sekta ya umma na sekta binafsi kuweka nguvu 
zao pamoja katika kuhakikisha wanachi wanapata huduma bora za afya.
Akielezea mkakati wa Mkoa dhidi ya
 jinsi gani Mkoa umejiandaa endapo atapatikana mgonjwa wa Ebola katika 
Mkoa wa Tanga, Kaimu Mganga  Mkuu wa Mkoa  wa Tanga Dr Asha Mahita 
amesema kuwa tayari maeneo mbalimbali yenye vifaa maalumu yametengwa ili
 kutoa huduma ya kitabibu kwa wagonjwa wa aina hiyo. Maeneo hayo ni 
pamoja na eneo la Masiwani lilipo jengo la Hospitali ya Wilaya ya Tanga 
na kituo kingine kipo Mpakani Horohoro.
Serikali pia imekuchukua tahadhali
 katika maeneo ya mpakani hasa eneo la Horohoro  mpaka wa Tanzania na 
Kenye na uwanja wa ndege kwa kuweka kifaa maalumu cha kuweza kupima na 
kutambua msafiri mwenye maambukizi ya  Ugonjwa wa Ebola. Hatua ambayo 
imefikiwa baada ya kusikia kuwepo mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za 
jirani na hasa Afrika.
Akifafanua dhana ya ushirikiano 
kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika kutoa huduma za afya, 
Dr.Samweli Ogillo ambaye ni Mtendaji Mkuu kutoka chama cha Watoa huduma 
Binafsi  Nchini ( APHFTA)amesema ni jambo la msingi iwapo Serikali na 
Sekta binafsi zitaweka nguvu ya pamoja ili kudhibiti na kuzuia ebola 
kuingia nchini kwa sababu upande mmoja peke yake hauwezi.
Hadi sasa hakuna mgonjwa yeyote 
mwenye dalili ya ugonjwa wa Ebola ambaye ameripotiwa kupatikana katika 
nchi ya Tanzania.  Historia inaonyesha mwaka 2012  Mwezi wa Julai 
ulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Ebola  magharibi mwa Uganda eneo linaitwa
 Kabaale ambapo zaidi ya watu 14 walipoteza maisha.
Ebola ni ugonjwa hatari 
unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu “Ebola 
Virusi na husambaa kwa haraka sana . Dalili zake ni pamoja na homa kali 
inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua, 
njia ya haja kubwa na ndogo, mdomoni, machoni kutapika na kuharisha 
damu. Stori & Picha na Monica Laurent, Afisa Habari Tanga

No comments:
Post a Comment