
Mkurugenzi
 wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) 
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho 
makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni 
Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed 
Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.

Mkurugenzi
 wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) 
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho 
makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni 
Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed 
Ramadhan wazamini wa maonesho hayo.

Mratibu
 wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan 
(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya 
maonesho makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. 
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion 
Elias.

Mkurugenzi
 wa Kampuni ya Insights Productions Limited, Marion Elias (kulia) 
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maonesho 
makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam. Katikati 
ni Mratibu wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed 
Ramadhan wazamini wa maonesho hayo na kulia ni Meneja Bidhaa za Azam, 
Abubakar Suleiman.
Dar es Salaam
KAMPUNI ya Insights Productions 
Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam Tanzania imeandaa maonesho 
makubwa ya keki yanayotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam na 
kuwakutanisha wadau mbalimbali wa uandaaji na utayarishaji wa keki. 
Maonesho hayo yatajulikana kama ‘Azam World of Cakes Exhibition’.
Akizungumza na vyombo vya habari 
leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions 
Limited, Marion Elias alisema maonesho hayo yanatarajiwa kuwakutanisha 
wadau mbalimbali binafsi, makampuni na taasisi waandaaji wa keki nchini 
Tanzania ikiwa ni sehemu ya kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu 
zaidi wa shughuli hizo.
Bi. Elias alisema dhumuni la 
maonesho hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika Desemba 6, 2014 jijini Dar 
es Salaam ni pamoja na kusherehekea taaluma ya uokaji keki kwa kuonesha 
ubunifu na utaalam wa utengenezaji na upambaji wa keki bidhaa 
inayopendwa na watu wengi na kutumika katika shughuli anuai za kijamii. 
Alisema washiriki wa tamasha hilo mbali na kushindanisha na kuonesha 
bidhaa zao za keki pia wanatarajia kupata semina ya mafunzo juu ya 
utengenezaji bora wa keki ikiwa na lengo la kuboresha zaidi taaluma zao.
Alisema washiriki hao pia 
watafanya maonesho ya utayarishaji wa vyombo vya kutengenezea keki, 
utayarishaji wa unga wa ngano kwa ajili ya kupikia keki, kutambua unga 
bora wa keki, uchanganyaji wa unga na viungo vingine kwa ajili ya 
uboreshaji wa radha ya keki.
Alisema maonesho mengine 
yatakayofanywa na wadau hao wa keki ni pamoja na uhifadhi bora wa keki 
kwa muda mrefu bila kuharibika na washiriki kuonesha maumbo mbalimbali 
ya keki yenye mvuto kwa watumiaji wa keki na jamii nzima.
Alisema maonesho hayo 
yanayodhaminiwa na Azam watengenezaji wa unga bora kwa ajili ya 
kutengenezea bidhaa hiyo, yatawashindanisha wadau wa uandaaji keki na 
pia washindi watakao tajwa na majaji wa maonesho watajipatia fedha
 taslimu na bidhaa mbalimbali.
“…Onesho hili litahusisha jamii 
yote inayojishughulisha na utengenezaji wa keki, upambaji wa keki, 
wauzaji wa keki na wanaojishughulisha na bidhaa mbalimbali zinazotumika 
kutengeneza keki kama vile unga wa ngano wa Azam,”
 alisema Mkurugenzi wa Insights Productions Limited, Bi. Elias.
Akifafanua zaidi Mkurugenzi huyo 
alisema onesho hilo litajumuisha bekari na hoteli mbalimbali, Vyuo vya 
taaluma ya hotelia toka Tanzania na majirani (Afrika Mashariki) pamoja 
na watengenezaji keki binafsi. Wananchi watakaotembelea maonesho hayo 
ambayo hayata kuwa na kiingilio watapata fursa ya kujionea aina na 
mitindo mbalimbali ya utengenezaji wa keki pamoja na kuonja bidhaa hiyo 
kwenye maonesho ambayo yatafanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia maonesho hayo Mratibu
 wa Matangazo na Uhusiano wa Umma wa kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan 
alisema Azam ikiwa ni kampuni inayotengeneza unga bora wa kutengenezea 
keki imeamua kudhamini ikiwa ni ishara ya kutambua taaluma hiyo ya 
uokaji keki nje na ndani ya Tanzania.
 *Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment