JIJI LA DAR ES SALAAM KUJENGEWA MFUMO WA KISASA WA UONDOAJI NA USAFISHAJI WA MAJITAKA PAMOJA NA MIUNDOMBINU MIPYA YA KUSAMBAZIA MAJISAFI MAENEO YASIYO NA MTANDAO WA MABOMBA.
Maeneo
mengine yatakayoguswa na mradi huo jijini Dar es salaam ni Msasani,
Kawe, Mbezi Beach, Kurasini,Keko, Chang'ombe, Temeke, Hananasif,
Tandale, Kijitonyama, Makumbusho, Mabibo, Ubungo, Manzese, Sandali,
Tandika na Miburani.Mhandisi
Lwenge amesema mradi huo wa kipekee utahusisha ujenzi wa mitambo mitatu
ya kisasa ya kusafisha majitaka katika maeneo ya Jangwani, Kurasini na
Mbezi Beach.
Aidha,
kupitia miradi hiyo mikubwa Serikali inaendelea kuishughulikia kero ya
uhaba wa maji katika maeneo ya Bunju,Mabwepande, Boko,Tegeta,Kunduchi,
Mbezi Beach, Mbezi Juu, Salasala, Kawe, Makongo, Mikocheni, Msasani,
Masaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Sinza, Manzese, Ubungo,
Mabibo, Kigogo, Buguruni na maeneo yote ya katikati ya jiji hilo.
No comments:
Post a Comment