Tutangaze vivutio vya kiutamaduni: Prof. Elisante Ole Gabriel
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Hassan Bendeyeko akifungua kikao
kati ya wadau wa Sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara
husika kilichofanyika Mjini Songea Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Afisa Elimu MkoaBw.Gharama
KinderuKatibu
Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo akisikiliza maelezo
ya baadhi ya vifaa vilivyotumika katika vita ya Majimaji kutoka kwa
Afisa Elimu Makumbusho ya Taifa Bi. Blantina Raphael wakati
alipotembelea makumbusho hayo mjini Songea, katikati ni Afisa Elimu wa
Mkoa wa Ruvuma Bw.Gharama Kinderu. picha na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ametoa wito
kwa viongozi na wadau wa sekta ya Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma kutangaza
Utamaduni na Utalii unaopatikana katika mkoa huo.
Wito huo
umetolewa jana mjini Songea na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa
akizungumza na wadau wa sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
“Mkoa wenu una vivutio
vingi vya asili vinavyoonesha tamaduni za wanaruvuma ambavyo vikitumika
vizuri ni fursa nzuri ya mapato” alisema Prof Gabriel.Ameongeza kuwa
Mkoa wa Ruvuma una vivutio vingi vya Utamaduni vya kuvutia watalii
ambavyo ni fursa nzuri ya kutangaza Utamaduni wa Mkoa na Tanzania kwa
ujumla.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan
Bendeyeko alikiri kuwepo kwa changamoto ya kuvitangaza vivutio hivyo
kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo .Hata hivyo alisema kuwa ujenzi
wa miundombinu utasaidia vivutio hivyo kufikika kwa urahisi na
wanategemea Mkoa huo kuinuka kiuchumi hasa baada ya changamoto hiyo
kutatuliwa.
Bw.Bendeyeko alisema kuwa baadhi ya vivutio vya
kiutamaduni vinavyo hitaji kutangazwa ili vifahamike ndani na nje ya
nchi ni pamoja na Makumbusho ya Majimaji, eneo waliponyongwa wapiganaji
wa vita vya majimaji, Ziwa Nyasa pamoja na mbuga mbali mbali.
Aidha
alieleza kuwa wanatarajia kuajiri Maafisa Utamaduni wakutosha katika
kila Halmashauri ambapo kwa kushirikiana na Maafisa Habari na waandishi
wa habari kutangaza vivutio hivyo
No comments:
Post a Comment