TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Thursday, June 2, 2016
Benki ya Barclays yatoa msaada wa madawati 70 Handeni.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto) akipokea sehemu ya madawati 70 kutoka kwa Meneja Masoko wa Benki ya B arclays Tanzania (BBT) Nasikiwa Berya yaliyotolewa ba benki hiyo kusaidia Shule ya Sekondari Handeni kupitia timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga hivi karibuni.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto), akikabidhi madawati hay kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Handeni wilayani humo hivi karibuni.
Meneja Masoko wa Benki ya B arclays Tanzania (BBT) Nasikiwa Berya (watatu kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa madawati 70 kwa Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari handeni, Amani Mmbaga, yaliyotolewa na benki kupitia timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga .
Mmoja wa maofisa wa Benki ya Barclays Tanzania, Raymond Bunyinyiga (kushoto), akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Barclays wakibeba madawati tayari kuyakabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Tanga kusaidia shule za sekondari wilayani Handeni.
Mchezaji wa timu ya soka ya Benki ya Barclays iitwayo ‘Blue Eagle’ Edwin Makata, akichuana na Issa Silaji (kulia) wa timu ya soka ya Shule ya Sekondari Handeni, katika mchezo wa kirafiki mara baada ya kukabidhi msaada wa madawati 70 yaliyotolewa na timu hiyo
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment