Na: Veronica Mwakimi.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini imezitaka halmashauri zote kuacha urasimu katika upatikanaji wa hati miliki ya makazi kwa watanzania waliopo kwenye maeneo mbali mbali kwa kuwa inachangia kuzolotesha maendeleo ya Wananchi na makazi yanayowazunguka .
Akizungumza na Jambo leo katika mahojiano maalum wa gazeti hili, Kaimu kamishina msaidizi wa Wizara ya Ardhi, bwana Idriss Kayera, amesema jijini dar es salaam leo kuwa wananchi wapewe elimu ya juu ya viambatanisho muhimu katika hatua ya upatikanaji wa hati hizo kwa watanzania ili kuweza kumiliki ardhi.
Bwana Kayera amesema kuwa Serikali kwa sasa inalenga kuongeza hati miliki ya ardhi kwa watanzania maeneo mbali mbali ya nchini kupitia halmashauri zinazojishugulisha na maeneo ya upimaji wa maeneo ya makazi ili kuendana na kasi hiyo ya mabadiliko.
hata hivyo ameongeza kuwa, kwa sasa Serikali inao mpango wa kuongeza hati miliki hizo kwa ajili ya kuwaweka watanzania kuweza kujimilikisha Ardhi tofauti na miaka ya nyuma ambapo watanzania wengi wameishi kwenye makazi yao bila kuwa na hati za umiliki wa ardhi hizo.
Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi
aidha ameyataja maeneo ambayo yametengwa bila utaratibu maalum kuwa ni pamoja na kimara ambayo unafanyika mpango wa kuweza kuyapima kama yalivyo huku pia akisema kuwa yapo maeneo yaliyojengwa pasipo utaratibu ikiwemo Buguruni, Tandika, Mburahati, Vingunguti ambako wakazi wake watapewa leseni ya makazi kutokana na msongamano walionao.
Mpaka sasa katika mwaka wa 2015/16 tayari wamepima hati miliki 23,000, ikiwa ni kwa maeneo ya mjini, na kuongea kuwa umuhimu wa hati miliki ni kumuwezesha mwananchi kuweza kujiendeleza yeye pamoja na Maisha yake ikiwa ataweza kuyatumia vyema makazi hayo pamoja na hati hiyo ambayo anaweza kuitumia kujiwekeza kwenye uchumi mkubwa tofauti na mkazi ambaye yupo kwenye makazi yasiyokuwa kwenye mipango miji.
Wizara ya ardhi imefikia maamuzi hayo ikiwa ni pamoja na kuwabana Makandarasi feki wanaojenga majumba bila utaratibu au kutokuwa na kibali kutoka kwenye halmashauri husika za mikoa vitendo vinavyopelekea kuhatarisha maisha ya wakazi wa maeneo husika pale majengo yanapokosa sifa na vigezo vya uimara wa ujenzi huo feki, ambapo pia imewataka kuacha mara moja kujichukulia hatua kiholela katika kujihusisha na ujenzi na badala yake wametakiwa kufuata utaratibu husika kutoka kwenye halmashauri hizo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment