Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib
alisema jana jijini Dar es SAlaam kuwa maandalizi yamekamilika na
Mbwana amewasili nchini kwa mechi ya timu ya TAifa ya Tanzania (Taifa
Stars) na Misri utakaochezwa Jumamosi.
Alisema sherehe hizo zitaambatana na ugawaji wa nyumba na misingi
ya nyumba kwa wasanii 35 ambao wanafikisha ya wanachama 180 waliokwisha
kabidhiwa nyumba zao.
Alisema SHIWATA imemzawadia Mbwana ekari tano ili ajenge kituo cha
michezo kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana wa Tanzania
watakaolitangaza taifa hili kwenye medani ya michezo kimataifa.
Taalib alisema mtandao huo unaomiliki eneo la ekari 300 za
kujenga makazi unawakaribisha wadau wa michezo kuwekeza kwa kujenga
kumbi za burudani,shule za michezo, studio za kurekodia, viwanda vya
kutengeneza vifaa vya michezo na hosteli za kufikia wachezaji.
Alisema sherehe za kugawa nyumba zinafanyika kwa mara ya tano
kutoka ujenzi huo uanze katika kijiji hicho ambapo wanachama 185
wamekabidhiwa nyumba zao walizojengwewa kwa njia ya kuchangishana.
Alisema mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa HAbari, Utamaduni
na Sanaa, NApe Mnauye ambaye atakuwa waziri wa pili kutembelea kijiji
hicho baada ya NAibu WAziri wake, Anna Wambura kutembelea mapema mwaka
huu.
Viongozi wengine waliowahi kutembelea kijiji hicho ni kiongozi wa
mbio za mwenge mwaka 2014, Wakuu wa wilaya ya Mkuranga wastaafu, Mercy
Silla, Clemency na Mkuu wa wilaya hiyo wa sasa, Abdallah Kihato.
Wageni wengine walioalikwa kwenye sherehe hizo ni Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ITFF), Jamal Malinzi viongozi wa
Serikali wa Wilaya ya Mkuranga na wasanii maarufu nchini.
No comments:
Post a Comment