Katibu wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO
Ndugu ADO SHAIBU akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam
kuhusu mapokezi ya kumpokea kiongozi yao na mbunge pekee wa chama hicho
ZITTO KABWE ambaye naye amekumbwa na timua timua ya bungeni,mapokezi
ambayo yatafanyika Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili
Na EXAUD MTEI
Story ambayo bado ipo maskioni mwa watanzania walio wengi ni
mwenendo wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania na mizengwe yake
ambayo imesababisha wabunge saba wa vyama vya upinzani kusimamiswa
kushiriki shughuli za bunge kwa vipindi Tofauti tofauti akiwemo mbunge
kutoka ndani ya chama cha Act wazalendo Mh ZITTO ZUBERI KABWE na wabunge
wa vyama vya UKAWA.
Sakata hilo limeendelea kuchukua Headline katika maeneo mbalimbali
ambapo asubuhi hii chama cha ACT wazalendo kupitia kwa kiongozi wao ADO
SHAIBU wamejitokeza mbele ya wanahabari kueleza msimamo wa chama chao
kuhusu sakata hilo.
Akizungumza na wanahabari leo Katibu huyo wa itikadi mawasiliano
na uenezi wa ACT ADO SHAIBU ameeleza kuwa chama hicho kimeandaa mapokezi
ya kiongozi wao ambaye amekumbwa na adhabu hiyo mapokezi ambayo
yanataraji kufanyika Jijini Dar es salaam na baadae kufwatiwa na mkutano
mkubwa wa hadhara ambao umepangwa kufanyika katika viwanja vya ZAKIEM
mbagala lengo likiwa ni kuwapa nafasi wabunge hao kueleza ukweli wa yale
yanayoendelea bungeni Dodoma.
Pamoja na mandalizi hayo chama hicho kimewaandikia barua makatibu
wa vyama vya upinzani ambao nao wanapinga adhabu hiyo kutoka
CHADEMA,CUF,na NCCR-MAGEUZI kuwaomba kuungana nao katika mapokezi hayo
ambayo yamepewa jina la OPERATION LINDA DEMOCRASIA na bado hawajapata
majibu yao lakini wanaamini wataungana nao katika Operation iyo ambayo
itafwatiwa na mikoa mingine takribani minne.
No comments:
Post a Comment