











Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini.
Madiwani wa halmashauri ya mji wa Kahama wameupongeza Mgodi wa
Dhahabu wa Buzwagi ulioko wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kwa namna
ambavyo umekuwa ukishiriki katika kutekeleza miradi mbalimbali ya
Maendeleo ambayo imekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Kahama na
hususuani vijiji vinavyozunguka Mgodi huo.
Pongezi hizo zimetolewa kwa niaba ya madiwani hao na mwenyekiti wa
halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija wakati wa ziara ya siku moja
iliyokuwa imelenga kujionea namna Mgodi huo unavyofanya shughuli zake za
uchimbaji.
“Kwa niaba ya halmashauri ya mji tunawapongezeni sana kwa namna
ambavyo mmekuwa chachu ya mendeleo kwa wilaya yetu na tunafarijika kwa
sababu leo mji wetu uko na barabara nzuri lakini pia wakazi wa
Mwendakulima na maeneo ya jirani wanao uhakika wa kupata huduma nzuri za
afya katika kituo cha afya ambacho mmeshiriki kukijenga, watoto wetu
pia wanaouhakika wa kusoma vizuri kutoka na miundo mbinu mlioiweka
katika baadhi ya shule na hasa ujenzi wa maabara za kisasa ” alisema
Shija.
Mwenyekiti huyo pia aliuomba uongozi wa Mgodi kuwezesha
upatikanaji wa kifaa kitakachosaidia mji wa Kahama kupata umeme wa
uhakika ambao utaendana na Mahitaji ya shughuli za kiuchumi kwa mji wa
Kahama kutokana na line iliyopo sasa kushindwa kukizi Mahitaji ya wakazi
wa mji wa huo.
Akijibu ombi hilo Meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa
Mwaipopo amesema mpaka sasa kifaa hicho kimeisha fika na kinachosubiliwa
ni wataalamu waliotengeneza kifaa hicho kutoka ujerumani kuja na
kukifunga.
“Kifaa kimeisha fika na tunachosubiri kwa sasa ni wataalamu tu
kuja na kukifunga, matumaini yetu ni kuwa kazi hiyo itakapokamilika
wananchi wa Kahama wataondokana na tatizo la umeme usiokuwa wa uhakika.”
Alisema Mwaipopo.
Ziara hiyo ambayo ilihusisha madiwani wa mji wa Kahama, Mbunge wa
Kahama mjini, Jumanne Kishimba na wataalamu wa halmashauri hiyo,
walipata fursa ya kutembelea maeneo mbali ya Mgodi huo na kuelezewa
namna suala la usalama wa mazingira linavyozingatiwa, ambapo madiwani
hao walishangazwa na namna Mgodi huo ulivyozingatia sheria mbalimbali za
mazingira na uchimbaji na kulifanya eneo hilo kuwa salama zaidi.
Madiwani hao waliomba mgodi huo kuongeza ufahamu kwa Jamii kwa
kuongeza ziara nyingi zitakazo husisha wananchi wa kawaida kwa lengo la
kuwafahamisha shughuli zinazofanywa na Mgodi hali ambayo wamesema
itasaidia kupunguza taarifa za uongo ambazo zimekuwa zikisambaa mitaani
kutokana na Jamii kutokujua ukweli.
No comments:
Post a Comment