Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson
akiendesha kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya Wabunge na Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi
wa Bunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania leo.
Wageni
mbalimbali waliolitembelea Bunge wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano
wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Baadhi
ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari St. Anne Marie ya Mbezi Beach jijini
Dar es salaam wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (kulia)
akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki ndani ya Ukumbi wa
Bunge, Dodoma leo.
Baadhi
ya Mawaziri Mawaziri wakifuatilia masuala mbalimbali ndani ya ukumbi wa
Bunge wakati wa kikao cha 36 cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania leo.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. Sulemani Jafo akijibu maswali ya wabunge wakati wa kikao cha 36 cha
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akichangia jambo kuhusu sekta ya Afya Bungeni mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwini Ngonyani akijibu maswali ya wabunge kuhusu uboreshaji wa Mawasiliano ya simu vijijini Bungeni mjini Dodoma.
Wageni mbalimbali waliolitembelea Bunge wakifuatilia kikao cha 36 cha mkutano wa 3 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.
Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Judith Wabura “Lady Jaydee” – (katikati) akiwa miongoni wa wageni waliolitembelea Bunge kujionea shughuli za kikao cha 36 cha Bunge mjini Dodoma leo.
Mbunge wa jimbo la Mwibala (CCM) Mhe. Kangi Lugola akiomba mwongozo wa Spika wakati wa kikao cha 36 cha Bunge mjini Dodoma leo.
Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Judith Wabura “Lady Jaydee” – (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi Mhe. Andrew Chenge (Kulia) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi nje ya ukumbi wa Bunge.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa Vijijini wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge wakiwa wameambatana na mwanafunzi mwenzao Eva Tolage (16) wa pili kutoka kushoto aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani akiwa miongoni mwa vijana 2 kati ya 40,000 ambao barua zao zilisomwa waliomtumia barua Rais huyo duniani kote kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi zao kuhusu upatikanaji wa Maji chini ya Kampeni ya Simama na EVA.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akimsalimia Mwanafunzi Eva Tolage (16) kutoka Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa Vijijini aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani akiwa miongoni mwa vijana 2 ambao barua zao zilisomwa kati ya 40,000 kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi zao kuhusu upatikanaji wa Maji chini ya Kampeni ya Simama na EVA.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassim Majaliwa akimsalimia Mwanafunzi Eliudi Sanyi wa Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa Vijijini akimsalimia wa Tanzania nje ya ukumbi wa Bunge, Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlowa iliyoko Iringa Vijijini ambao wako kwenye kampeni ya Simama na Eva, Mwanafunzi wa Shule hiyo (katikati) aliyemwandikia Barua Rais Barack Obama wa Marekani kati ya 40,000 kuomba viongozi wa dunia kutekeleza ahadi kuhusu upatikanaji wa Maji.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akisalimiana na Msanii wa kizazi kipya Vanessa Mdee nje ya Ukumbi wa Bunge leo. Katikati ni Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akizungumza jambo na Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira nje ya Ukumbi wa Bunge, Dodoma.Picha/Aron Msigwa –DODOMA
No comments:
Post a Comment