TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Monday, May 30, 2016
WAZIRI MKUU ANATARAJIWA KUFUNGUA MKUTANO WA KULINDA URITHI WA DUNIA.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix (katikati) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha leo ambako May 31, 2016 anatarajiwa kufungua mkutano wa Kimataifa wa 'Africa World Heritage' kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha -AICC.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na Woinde Shizza,Arusha
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa kesho anatarajiwa kufungua mkutano wa kulinda urithi wa dunia wa Afrika kama nyenzo ya maendeleo endelevu utakao fanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha unaotarajiwa kufanyika kwa siku nne .
Akiongea na waandishi wa habari katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi wakati akiongea na waandishi wa habari jijini hapa juu ya maandalizi ya mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa serekali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na shirika la UNESCO nakituo chake cha urithi wa dunia.
Alisema kuwa madhumuni ya mkutano huo ni kutambua changamoto na mambo ambayo yanatishia na kuadhiri uhifadhi bora wa maeneo ya urithi wa dunia katika afrika .
Aidha mkutano huo utapendekeza suluisho kwa kupitia upya shughuli zinazotekelezwa katika eneo la urithi wa dunia na kuangalia mchango wa miradi ya jamii za kiafrika na kuandaa muelekeo wa miaka kumi ijayo.
Milanzi alisema kuwa mkutano huo utapendekeza suluhisho kwa kushawishi wanawake kuongeza ushiriki wao katika miradi inayoendana na uhifadhi wa urithi na maendeleo endelevu pamoja kuchunguza jinsi mitafaruku inayotokea kwenye maeneo urithi wa dunia kutokana na makundi ya kigaidi na kutunza amani utamaduni na uridhi asilia.
Aliongeza kuwa pia mkutano huo umejikita kwenye sera ya UNESCO ya mwaka 2015 inayohusu kujumuisha maendeleo endelevu kwenye mkataba wa uridhi wa dunia.
“mkutano huo pamoja na matokeao tegemewa kisayansi, pia uatakuwa na manufaa kwa taifa na sio tu kuitangaza Tanzania kutalii na kisasa bali pia ni fursa muhimu ya kiuchumi kutokana na idadi ya wageniwatakao uthudhuria mkutano huu pamoja na kuanzisha mitandao wa kitaaluma na kujenga mataji wa kijamii”alisema Malinzi
Aidha pia mara baada ya mkutano huu na kupata muafaka wa yote kutakuwa na tamko lililotokana na majadiliano yaliyokuwa yakifanyika siku zote za mkutano na tamko hili linatarajiwa kutolewa katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment