Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza wakati wa
uzinduzi wa wiki ya mazingira duniani ambapo manispaa ya Ilala kwa
kushirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd na nyingine kwa
kufanya usafi katika fukwe za bahari ya Salender jana jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga,
Victor Muneni na kulia ni Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa
ya Ilala Bw. Abdon Mapunda.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni
akizungumza jambo na wadau wa mazingira waliokusanyika kwenye viwanja
vya Salender Club kabla ya kuanza zoezi la usafi wa mazingira.
Baadhi ya wadau wa mazingira kutoka ofisi za Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala, makapuni ya usafi yaliyopewa zabuni ya kusafisha
manispaa ya Ilala ikiwemo Green Waste Pro Ltd, Vijana kutoka Roots and
Shoot waliokusanyika kwenye uzinduzi wa wiki ya mazingira duniani
iliyozinduliwa jana duniani kote.
Kiongozi wa dhehebu la Dawoodi Bohra nchini, Bw. Zainuddin Adamjee
(wa pili kushoto) akimtambulisha Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi
Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin (wa tatu
kushoto) kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) mara baada
ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,
Balozi Joseph Sokoine (kushoto) akitoa salamu za serikali kwa Kiongozi
Mkuu wa dhehebu la Bohora duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb
Saifuddin aliyewasili jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akielezea mipango ya
manispaa ya Ilala katika kuweka jiji safi wakati wa hafla fupi ya
kukabidhiwa 'Dustbin' 53 zilizotolewa na Burhani Foundation Tanzania
iliyofanyika katika mskiti wa dhehebu la Mabohra nchini.
Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar
Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin moja ya Dustbin kati ya 53
zilizotolewa na Burhan Foundation kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Kiongozi huyo jijini
Dar es Salaam.
Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar
Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin akimvisha kikoi Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Raymond Mushi na kumwombea dua baada ya kukabidhi Dustbin 53 kwa
ajili ya manispaa ya Ilala.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akimshukuru Kiongozi Mkuu
wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb
Saifuddin kwa zawadi ya kikoi.
Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon
Mapunda akipokea zawadi ya kikoi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa dhehebu la
Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin.
Mwenyekiti wa CCM, Serikali za Mitaa Kata ya Kisutu, Mustaquim
Darugar (kushoto) akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond
Mushi.
Ikiwa ni wiki ya mazingira duniani, Wilaya ya Ilala imeeleza
mipango yake ya kuweka mazingira katika hali ya usafi kusambaza makasha
yatakayotumika kuhifadhia taka baada ya kupokea msaada wa makasha 53
kutoka Taasisi ya Burhani.
Akipokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
alisema wilaya yake imeanza kujipanga katika hilo ili kuweka mazingira
safi na kuwataka wananchi wote kutupa taka katika makasha hayo mara tu
baada ya kumaliza matumizi yao.
Alisema jukumu la kuweka mazingira katika hali ya usafi nila kila
mmoja hivyo kila mtu ana wajibu wa kushiriki kuweka mazingira
yanayomzunguka katika hali ya usafi jambo ambalo linaweza kusaidia
kuondokana na magonjwa ya mlipuko ambayo mara nyingi yamekuwa
yakisababishwa na uchafu uliosambaa katika mazingira yanayotuzunguka.
“Kwa wananchi wote hata kama ukinywa maji au kula embe, ndizi na
hata kama ni vocha au umetumia sigara uchafu wote uwekwe katika makasha
hayo ili tuweze kuweka wilaya katika usafi na uchafu huo utakuwa unakuja
kuchukuliwa na watu ambao tumewaweka kufanya kazi hiyo,
Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon
Mapunda (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
(katikati) kuzindua wiki ya mazingira duniani pamoja na kuzungumza na
wakazi wa mtaa wa Sea-View pamoja na wafanyakazi wa makampuni ya usafi
ikiwemo Geen Waste Pro Ltd. Kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
Sea-View Upanga, Victor Muneni.
“Wilaya yetu imejipanga kwa sasa kusambaza makasha katika
mazingira yetu na katika kata zote ni wajibu wa kila mmoja kushiriki
kuweka mazingira katika hali ya usafi uchafu wote unatoka katika
mazingira yetu hatuna budi kushirikiana kufanya usafi,” alisema Raymond.
Kwa upande wa Taasisi ya Burhani ambao ndiyo wametoa msaada
kupitia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohra, Muslim Hassuji alisema wametoa
msaada huo ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Magufuli kuweka
mazingira katika kusaidia kuweka mazingira safi na pamoja na msaada huo
pia wamejipanga kuendelea kutoa msaada wa vifaa katika maeneo mengine ya
jiji la Dar es Salaam.
“Tunamuunga mkono Rais wetu Magufuli ili tuweke mazingira yetu
safi, msaada huu wa makasha ya kuhifadhia taka 53 kwa wilaya ya 53 ni
awamu yetu ya kwanza na tutaangalia jinsi yatakavyofanya kazi na baada
ya hapo tutatoa mengine na baadae tugawe hata kwa mkoa wote wa Dar es
Salaam,” alisema Hassuji.
Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafi ya Green West Pro Limited,
Anthony Mark aliwataka Watanzania wabadilike na kuwa na kujiwekea
utaratibu kuweka mazingira yanayowazunguka safi kutokana na wengi wao
kujisahau kufanya usafi.
“Watanzania wengi sio wastarabu unakuta mtu yupo ndani ya gari
anakunywa hata maji akimaliza anatupa kopo nje hii sio tabia njema
inatakiwa ifike hatua tubadilike na tushiriki kuweka mazingira yetu safi
sio wengine wanafanya wengine hawashiriki,” alisema Mark.
Aidha Mkurugenzi huyo wa Green West Pro aliwatupia lawama Shirika
la Umeme nchini (TANESCO) kwa tabia ya kuacha miti ambayo wamekuwa
wakikata kwa madai ya kuwa karibu na nguzo za umeme na baadae kuiacha.
Alisema sio ustaarabu kwani kufanya hivyo ni kuchafua mazingira na
kuwaachia wananchi uchafu ambao haukusababishwa na wao na hivyo
kuwataka kubadilika ili kusaidia kuweka mazingira safi kama jinsi Rais
Magufuli anavyoagiza.
Nae Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira kutoka Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda alisema kuelekea kilele cha wiki ya
mazingira wataendelea kushiriki katika maeneo mbalimbali kufanya usafi
ikiwa ni kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ambapo kwa
kuanza hapo jana Jumatano walishirikiana na Kampuni ya Usafi ya Green
West Pro ltd ambapo walifanya usafi katika eneo la Salender Bridge.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akitoa maagizo kwa Kamanda
wa kituo cha Polisi Salender Bridge kuhusiana usafi wa mazingira
kuzunguka maeneo yao katika fukwe za bahari ya Salender.
Mkaazi wa mtaa wa Sea-View mzee Peter Kabelwa almaarufu kama Mzee
Mzungu akishiriki zoezi la kuondoa uchafu uliozunguka katika fukwa za
bahari ya Salender Bridge.
Mwanamazingira kutoka Roots and Shoots akishiriki kukusanya taka zilizosambaa kwenye eneo la fukwe za bahari ya Salender Bridge.
Mkurugenzi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Anthony
Mark Shayo na Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Abdallah Mbena (kulia)
wakishirikiana na wafanyakazi wa kamouni hiyo kufanya usafi kwenye eneo
la fukwe za bahari ya Salender Bridge.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na wadau wa mazingira wakiendelea na zoezi la usafi kwenye fukwe hizo.
Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon
Mapunda (katikati) akishiriki zoezi la usafi kwenye fukwe za bahari ya
Salender Bridge.
Eneo hili lilisahaulika kwa muda mrefu bila kufanyiwa usafi kitu ambacho ni hatari kwa samaki wanaoishi kwenye fukwe hizo.
Muonekano wa fukwe za bahari ya Salender Bridge kabla ya kusafishwa na wadau wa mazingira wakiwemo Green Waste Pro Ltd.
No comments:
Post a Comment