TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Thursday, June 2, 2016
Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli,
Mhandisi Norbert Kahyoza
.
Na Rhoda James
Imeelezwa kuwa uelewa juu ya upatikanaji wa ardhi, Ushiriki wa wananchi na ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaohamishwa ili kupisha mradi wa bomba la mafuta litakalo jengwa kutoka kabaale nchini Uganda hadi Tanga Tanzania vitachangia katika kufanikisha zoezi la upatikanaji wa ardhi na kukamilisha shughuli za kimazingira kwa ajili ya ujenzi wa bomba hilo.
Hayo yameelezwa hivi karibuni mjini Dar es Salaam na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Mhandisi Norbert Kahyoza wakati wa Warsha iliyolenga kujadili upatikanaji wa ardhi na kutathimini athari za Mazingira (EIA) ya ujenzi wa bomba hilo la mafuta kwa serikali ya Tanzania na Uganda.
“Serikali kutoka pande zote mbili lazima tuwe makini kuhusu upatikanaji wa ardhi, lazima wananchi wapate uelewa mzuri na waone uwepo wa umuhimu wa bomba hili la mafuta na faidi zake kwani mradi huu ni muhimu.” alisema mhandisi Kahyoza.
Aidha, Mkurugenzi wa Mkondo wa Chini kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. Wellington Hudson alieleza kuwa warsha hiyo ya upatikanaji wa ardhi pamoja na masuala ya mazingira ni ishara nzuri ya mwanzo katika utekelezaji wa mradi huo wa bomba la mafuta.
Vile vile mwakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya Uganda, Francis Elungat alisema kuwa Waganda wamekuwa wakijiuliza ni lini watafaidika na mafuta yao, hivyo amefurahishwa kuona kuwa mradi huo uko mbioni kuanza hivyo wananchi wa Uganda kufaidika na mafuta yao.
Ujumbe kutoka Uganda wakifuatilia Mada zilizowasilishwa katika kikao cha wadau wa mafuta, kutoka kulia ni afisa Mwandamizi wa Mazingira, Jane Byaruhanga, wa pili ni afisa Mwandamizi wa Ardhi, Francis Elungat na afisa mwandamizi wa Ardhi Denis Karamagi.
Mchakato wa upatikanaji wa ardhi na kushugulikia masuala ya mazingira ni hatua za awali za safari ya wananchi wa Uganda kupata faida za mali asilia inchini mwao.
Aliongeza kuwa ujenzi wa bomba la mafuta na kiwanda cha kuchakata mafuta hayo ni muhimu sana kwa wananchi wa Uganda na nchi nyingine za Afrika Mashariki hivyo ni vema pande zote mbili zikubaliana katika hatua zote za utekelezaji wa mradi huo.
Naye Meneja wa Mradi wa Kampuni ya Total Uganda, Jean Luc Bruggeman, alisema kuwa ni lazima kuwepo na maelewano ya pamoja kwa pande zote mbili juu ya nini kinahitajika na taratibu za upatikanaji wa cheti cha mazingira (EIA) ili kuwezesha kuanza shughuli za ujenzi wa mradi mapema, na kinachotarajiwa kufanyika kulingana na makubaliano ya nchi hizo mbili na kuelewana nani atafanya nini katika mradi huo.
Wajumbe wakifuatilia mada katika kikao cha wadau wa Bomba la mafuta kilichofanyika katika hotel ya New Africa jijini Dar es Salaam.
Warsha hiyo ilihudhuriwa na Ujumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Uganda, Kampuni ya Total E&P Uganda, wajumbe kutoka Halmashauri yaTanga, Bandari ya Tanga na Dar es Salaam, Shirika la Reli Tanzania,Wizara ya Fedha, Wizara ya Ardhi, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiziwa Mazingira (NEMC),Chuo cha Ardhi, Tanroads, Ofisi ya MwanasheriaMkuuna Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment