Waziri wa Maliasili Prof. Jumanne Maghembe akizungumza katika hafla ya
makabidhiano ya ndege maalum aina ya drones zilizotolewa na Mfuko wa WWF kusaidia
doria za kiitelijensia za kupambana na ujangili katika pori la akiba la Selous. Wengine katika picha ni Mkurugenzi
Mkuu wa Kimataifa wa Mfuko wa Uhifadhi Wanyamapori na Mazingira Duniani (WWF)
Dkt. Marco Lambertini (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji WWF – Ujerumani,
Ebenhard Brandes (kushoto).
Alieleza
kuwa changamoto kubwa inayoikabidili hifadhi ya Selous ni ujangili ambao kwa
kiasi kikubwa umesababisha idadi ya Wanyamapori hususani tembo kupungua kwa kasi
kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Alisema
kuwa takwimu zinaonesha kuwa mwaka 1986 idadi ya tembo katika pori hilo ilikuwa
50,000, idadi ambayo iliongezeka mwaka 2003 na kufikia 70,000 baada ya
Serikali ya Ujerumani kusaidia kuanzishwa kwa Mpango wa Kuendeleza Selous
(Selous Conservation Program) na Serikali ya Tanzania kukubali aslimia 50 ya
makusanyo yanayotokana na utalii yabaki kuendeleza uhifadhi katika pori hilo.
Alisema
kuwa baada ya mradi huo kuisha na mfumo wa “retention” kuondolewa na Serikali
hali ilibadilika na kuwa mbaya zaidi ambapo kati ya mwaka 2008 na 2011 vitendo
vya ujangili viliongezeka maradufu, sensa ya mwaka 2013 ilionesha idadi ya
tembo hao kupungua hadi kufikia 13,000.
Prof.
Maghembe aliongeza kuwa pamoja na hayo Serikali imejipanga kuhakikisha
Wanyamapori wanalindwa usiku na mchana na kwamba wale wote wanaojihusisha na
vitendo vya ujangili watakamatwa na kufikishwa mahamani ili sheria ichukue
mkondo wake.
Prof.
Maghembe ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine ili kukomesha ujangili ni lazima
mataifa yaliyoendelea ambayo ndiko yaliko masoko makubwa ya meno ya tembo na
bidhaa zake kusitisha kabisa uingizwaji wa meno hayo katika nchi zao ili
kukomesha biashara hii haramu.
“Kuna
nchi ambazo tayari zimechukua hatua ya kukataza kabisa uingizwaji wa meno ya
tembo nchini mwao, mfano Marekani, tunaiomba sana jumuiya ya kimataifa wakiwemo
marafiki zetu China na nchi nyingine wakatae kabisa uingizwaji wa meno haya
nchini mwao, hii itasaidia sana kukomesha biashara hii haramu” Alisema.
Katika
hatua nyingine Prof. Maghembe aliwataka wafugaji walioingiza mifugo katika
maeneo yote ya hifadhi nchini waondoe mifugo yao kwa hiari kabla ya
kushinikizwa kufanya hivyo na Serikali kwa mujibu wa sheria.
Sheria ya
Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 Ibara ya 18 (2) inasema “Si ruhusa mtu yeyote
kuingia na kulisha mifugo ndani ya Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Ardhioevu”
Prof.
Maghembe alisema kuwa “mtandao wa ujangili unaanzia na watu wanaoingiza mifugo
ndani ya hifadhi, hivyo ni lazima sheria zifuatwe na waondoke mara moja,
watakaokaidi sheria itafuata mkondo wake na mifugo itakayokamatwa itataifishwa
na Serikali kwa mujibu wa sheria za nchi, sheria hizi hazina tofauti na sheria
zinazokataza watu wasijenge mabondeni au kwenye hifadhi za barabara”
Awali
akitoa
taarifa, Meneja wa Pori hilo la Akiba la Selous Mabula Misungwi
alieleza baadhi ya changamoto kuu zinazoikabili hifadhi hiyo kuwa ni
pamoja na ujangili, miundombinu mibovu ya barabara kwa ajili ya doria na
vifaa
ikiwemo magari ya doria na nyumba za watumishi.
No comments:
Post a Comment