WAZIRI Amina Salum Ali akiangalia vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen lililopo Saateni mjini Zanzibar.
BAADHI ya vyakula vilivyohifadhiwa katika ghala la kampuni ya Evergreen Saaeteni mjini Zanzibar.
MENEJA Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Khalid Ali
Yussuf, akimpa maelezo Waziri Amina Salum Ali juu ya uzalishaji wa
chakula alipotembelea ofisini kwake Mtoni nje kidogo ya mji wa
Zanzibar.
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akiwa katika
maeneo ya kiwanda cha Zanzibar Miling Corporation Mtoni alipofanya
ziara maalum kwa ajili ya kuangalia hali ya chakula nchini wakati huu wa
kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan.
WAZIRI wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali akioneshwa
ngano na Meneja Mkuu wa kiwanda cha Zanzibar Milling kilichoko Mtoni
Zanzibar Khalid Ali Yussuf, katika sehemu ya usagishaji alipotembelea
kiwanda hicho.
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Evergreen Abdulghafar Ismail Mohammed
akimfahamisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Amina Salum Ali juu
ya hali ya chakula nchini alipotembelea katika ghala lake Saateni mjini
Zanzibar.
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Bopar Enterprises Said Nassir Said,
akizungumza na Waziri Amina Salum Ali wakati Waziri huyo alipomtembelea
ofisini kwake Mombasa mjini Zanzibar.PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR –
HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment