TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Monday, May 30, 2016
Vijana nchini watakiwa kuwa huru kutoa maoni yao-jk
Na: Frank Shija, MAELEZO
Vijana nchini watakiwa kuwa huru kutoa maoni yao na wanapo kosea wawe tayari kukosolewa na kukujirekebisha.
Rai hiyo imetolewa na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa mahafali ya Pili ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika jana katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kikwete alisema kuwa vijana wanapaswa kutoogopa kukosea, kwani watu ujifunza kutokana na makosa hivyo ni vyema wakathubutu kufanya mambo kwa kuzingatia misingi, weledi na kwa uwazi huku wakiepuka migawanyiko.
Wakati huo huo Kikwete ameahidi kulisaidia Shirikisho hilo kandana ya Dar es Salaam jumla ya shilingi milioni 20 kwa ajili ya kusaidia katika kutekeleza mradi wao wa kilimo na ufugaji wa kuku.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah alisema kuwa katika kuenzi na kutambua juhudi za Rais msataafu Jakaya Kikwete katika kusaidia Vijana wataanzisha Tuzo maalumu kwa Vijana zitakazo julikana kama “Jakaya Mrisho Kikwete Youth Awards”.
Ambapo lengo lake ni kuhamasisha viongozi waendelee kusthamini michango ya vijana katika kukuza na kuendeleza Taifa letu.
Shirikisho la Wanafunziwa Vyuo Vikuu (CCM) Seneta ya Dar es Salaam linaundwa na jumla ya matawi 34ambapo katika mahafali hayo ya pili jumla ya wahitimu 640 walitunukiwa vyetikutambua mchango wao katika kuimarisha uhai wa Chama chao vyuoni
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment