Hawa ni wanafunzi Miongoni mwao wapo walioweza kuathirika na timua hiyo leo wamelazimika kukutana na vyombo vya habari katia kujadili suala hilo ambalo mpaka sasa hakuna mwenye tamko la mwisho zaidi ya mheshimiwa Rais wa jamhuri waTanzania. na hii ndiyo barua ambayo leo imewasilishwa kwa baadhi ya Wandishi wa habari ikielezea jinsi Tanzania inavyotaka kukiuka Misingi ya haki za Binadam na haki ya Utawala Boba.
(Picha kwa Hissan ya Miss Demokrasia Tanzania
=========================================
Press Release
Ndugu
Waandishi wa habari,
Awali
yayote tunapenda kupongeza jitihada kadha wa kadha ambazo zimekuwa zikifanywa
na serikali kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha inaboresha mfumo wa Elimu
nchini.
Pamoja na ukweli
kwamba, kumekuwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Elimu haswa katika awamu hii ya Uongozi
wa Mh. Raisi, John Pombe Makufuli. Mtandao wa Wanafunzi Tanzania unasikitishwa
na kulaani baadhi ya maamuzi yaliyokwishafanyika na kukiuka utu, haki za
Wanafunzi na vile vile taratibu, kanuni na sheria za nchi hii.
Kuhusu
Sakata la Kufukuzwa Wanafunzi UDOM
Mumesikia
hoja za viongozi mbalimbali juu ya sakata la Wanafunzi Waliosimamishwa UDOM,
mmesikia hotuba ya Mh. Joyce Ndelichako, Waziri mwenye dhamana katika wizara ya
Elimu, lakini vile vile mmesikia hotuba ya Mh. Raisi, John Pombe Makufuli
aliyoitoa akiwa chuo kikuu cha taifa (UDSM)
tar. 02.06.2016
Tangu tar.
28 mei 2016, mara baada ya agizo la Serikali kupitia Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi (MoEST) la kuwarejesha nyumbani
Wanafunzi takribani 7802 Mtandao huu umekua ukifanya tafiti za kina kupitia
idara yake (Reseach& Training Department) na kupata taarifa za pande zote
mbili kutoka vyanzo mbalimbali vya taarifa “Wahanga(Wanafunzi waliofukuzwa) na
Watawala(Wizara ya Elimu) ”. Tumejiridhisha
kwamba kitendo kilichofanywa dhidi ya Wanafunzi wa UDOM ni ukiukwaji mkubwa wa
haki za Wanafunzi ambacho kilikuwa kwanza cha kimabavu na hakikuzingatia kabisa utu wa Wanafunzi husika. Taarifa zilizotufikia ni kwamba Wanafunzi
walifukuzwa kama Wakimbizi ndani ya nchi yao, Polisi walizagaa kila kona na
bunduki zao kama wanafukuza majambazi, hofu ilitanda na wanafunzi wengine
kuogopa kurudi chuoni kwa hali ilivyokuwa. Mtandao huu unasikitishwa kwa
matumizi makubwa ya vyombo vya dola lakini vile vile madhara yaliyowakumba
Wanafunzi husika wakati wa zoezi la kuwaondoa chuoni.
Chimbuko
la Mgogoro:
Ikumbukwe, wakati wa
uongozi wa Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa
Elimu kama vile Mamlaka ya Elimu (TEA), Tume ya vyuo vikuu (TCU), Mamlaka ya
vyuo vya Ufundi (NACTE) na wadau mbali mbali a Elimu, waliadhimia na kuzindua
program maalumu ya kusomesha waalimu wa masomo ya Sayansi katika shule za
sekondari nchini ili kutatua changamoto za uhaba wa waalimu wa masomo ya
sayansi. Lakini ili kupata waalimu wenye sifa Serikali ikaweka sifa za Udahili
kwamba itakuwa kwa wahitimu wa kidato cha nne tu waliopata daraja la 1,2 na 3
pia wawe na ufaulu wa alama A” au B” kutoka masomo ya sayansi. Na serikali
ikawashawishi kwa ahadi ya kuwapa mkopo kwa 100%.
Tumeshangazwa
kwamba, Sababu za kusimamishwa masomo wanafunzi hawa
zimeendelea kubadilika badilika, sababu ya kwanza
kabisa, ambayo ilisemwa na Prof. Joyce Ndelichako Bungeni ni Mgomo
wa Wahadhiri uliotokana na kukosa posho za kuwafundisha Wanafunzi
husika, Sababu ya pili ni wanafunzi
kukosa sifa.
Mtandao huu umejiuliza,
Kama suala kuu ni vigezo kwanini serikali isingeweka utaratibu maalumu wa
kuwaondoa wanafunzi wasio na sifa na kuwawajibisha
wale waliowadahili kinyume na standard zilizowekwa na serikali?
Ombi
letu.
2. Kama hotuba ya Mh. Raisi hapo juzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, akikiri kwamba kunawanafunzi wasio na vigezo walidahiliwa. Mtandao huu unaomba waliohusika kuwadahili wawajibishwe haraka iwezeanavyo lakini vile vile wanafunzi wafidiwe Rasilimali fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni.
Hatma
ya Wanafunzi (UDOM)
Kama itatokea,
kunamwanafunzi au kundi Fulani la Wanafunzi, halitopewa haki zake, Mtandao huu
utashirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu zikiwemo azaki zinazojihusisha na
masuala ya utetezi kisheria kutafuta haki za Wanafunzi husika mahakamani
Chanzo
cha Migogoro katika Sekta ya Elimu Nchini.
v Kutokuwa na Muafaka wa Kitaifa
katika Mfumo wa Elimu.
Mtandao huu unaamini
kwamba haya yote ni madhara ya kutokuwa na muafaka wa kitaifa/Msimamo wa itaifa
katia Sekta ya Elimu nchini. Kwa mda mrefu, mfumo wetu wa Elimu, Sekta
ya Elimu nchini imekuwa inaendeshwa na kiwango cha utashi wa Waziri wa Elimu
aliyepo madarakani na sio kuongozwa na dira/Muafaka/Msimamo wa kitaifa
katika sekta ya Elimu.
Tumeshuhudia, Mawaziri
wa Elimu tofauti tofauti, katika awamu tofauti tofauti za uongozi tangu uhuru
wa nchi hii (Mh.Jumanne Maghembe, Mh, Joseph Mongai, Mh. Shukuru Kawambwa na
sasa Mh. Joyce Ndalichako), wakifanya maamuzi kutokana na kiwango cha utashi
wao na mapenzi yao. Hii ni hatari katika taifa letu na imesababishwa na ukweli
kwamba taifa limekosa dira/Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini.
Hitimisho.
Mtandao wa Wanafunzi
Tanzania unaamini kwamba kilichotokea Chuo Kikuu cha DODOMA kitakuwa msingi wa
Serikali kupitia Wizara ya Elimu kuanza harakati rasmi za kimapinduzi za
kuunganisha wadau wote wa Elimu nchini ili kuwa na mjadala mpana wa kitaifa wa
namna ya kufikia Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini.
Vile vile Mtandao huu umeshaandaa waraka
maalumu kwa Waziri wa Elimu unaotoa muongozo wa namna taifa litakavyofanikisha
kuwa na Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini ambao tutauwasilisha
wizarani mapema wiki ijayo.
Mwisho kabisa, tunaomba
viongozi wote wa dini na wale wanaoamini, kuendelea kumwombea Mh. Raisi n a
viongozi wengine ili waongoze taifa hili kwa hekima na busara na kwa kufuata
taratibu, kanuni na sheria za nchi hii.
No comments:
Post a Comment