Klabu ya Rotary ya Oyster Bay Yatoa Huduma za Afya kwa Wanafunzi zaidi ya 950 wa Shule Mbili za Msasani
Dakitari wa macho akiwa katika jukumu la kumpima macho mwanafunzi wa shule ya msingi msasani
Rais wa klabu ya Rotary ya Oyster bay jijini Dar es Salaam, Bwana Mohammed Versi akizungumza na wanahabari
Baadhi ya madakitari wakiwa katika majukumu yao ya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata matibabu
Klabu
ya Rotary ya Oyster Bay ya jijini Dar es Salaam imeandaa kambi ya
matibabu na kutoa huduma za afya kwa wanafunzi wa shule mbili za
Msasani, Msasani A na Msasani B na kufanikiwa kutoa huduma kwa wanafunzi
zaidi ya 950. Kambi hiyo ya siku moja ilitoa vipimo vya afya, ushauri,
matibabu na huduma mbalimbali za meno, macho, malaria, usafi wa mwili,
minyoo, masikio, pua na koo (ENT), pamoja na magonjwa ya ngozi. Kampeni
ya Damu Salama pia ilifanyika wakati wa kambi hiyo ili kuwawezesha
uchangiaji wa damu katika benki ya damu salama.
No comments:
Post a Comment