Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez
akizungumza katika mkutano wa Baraza Kivuli la Umoja wa Mataifa kuhusu
Vijana kutoka nchi nane Afrika uliofungwa jana kwenye makao makuu ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha .

Mratibu wa Kongamano hilo Marx Chocha akizungumza jambo kwenye mkutano huo.

Vijana wakisikiliza kwa makini mada mijadala iliyokua inatolewa.

Ushiriki wa vijana wa kike ulipewa umuhimu wa kipekee katika
mkutano huo na walionesha uwezo wao katika kujadili masuala mbalimbali
yakiwemo ajira ,usalama na amani na mabadiliko ya tabia nchi.

Mshiriki kutoka Zanzibar,Asma Omar akipokea zawadi yake baada ya
kuibuka mshindi katika kusambaza habari za mkutano kwa njia ya mitandao

Mshiriki kutoka jijini Dar es Salaam,Lilian Kimani akipokea cheti
chake baada ya kutambuliwa kufanya vizuri kama mkuu wa Itifaki kwenye
mkutano huo.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodriguez akimkabidhi mmoja wa vijana cheti cha kutambua mchango wake .
SERIKALI YAAHIDI KUVIPATIA MAJI VIJIJI VINAVYOZUNGUKA BOMBA KUU LA MAJI LA ZIWA VICTORIA NA MAENEO YA PEMBEZONI MWA TANZANIA.

SHINDANO LA MAISHA PLUS MSIMU WA 5 LAZINDULIWA RASMI, KUONYESHWA MOJA KWA MOJA NA AZAM TV
Mkurugenzi
wa Azam Media Tido Mhando (Kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Maisha Plus East Africa Mkurugenzi wa Maisha Plus East Africa msimu wa
5 ambapo shindano linatarajiwa kuanza hivi karibuni itakapotangazwa
ratiba ya kutafuta washiriki wa shindano hili mikoani na nchi zingine za
Afrika Mashariki, kulia ni mmoja wa waandaji wa shindano hilo Bw.
Masoud Kipanya, Masoud Kipanya ni miongoni mwa waanzilishi wa Maisha
Plus na mtangazaji wa kipindi hicho ambacho huandaliwa na kampuni ya
DMB Company Limited na mwaka huu inandaa kwa udhamini mkubwa wa Azam
Media, Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jana katika studio za Uhai
Productions – Azam, Tabata jijini Dar es salaam.
Joyce Fisoo Katibu Mtendaji wa bodi ya filamu Tanzania akizungumza
mawili matatu wakati wa uzinduzi huo kama mgeni mwalikwa lakini pia kama
mdau muhimu wa shindano hilo.
Baadhi ya waandaji wa shindano la Maisha Plus kulia Francis Bonga na
David Sevuri wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo iliyofanyika
jana.Jikho Man na Vitalis Maembe wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo
iliyofanyika jana.

Mwanahabari na Bloger John Bukuku akihojiwa na mtangazaji wa Azam Tv
Benerick ambaye pia alikuwa ni mmoja wa washiriki wa msimu uliopita wa
Maisha Plus.
=============================================
MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YALIYOANDALIWA NA AGRIPROFOCUS YAFANYIKA UWANJA WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI.

No comments:
Post a Comment