TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 24, 2014

Bunge lijalo liiwajibishe serikali kwa kutokutekeleza maazimio ya bunge.

Umoja wa katiba ya wananchi Ukawa umelitaka bunge lijalo liiwajibishe serikali kwa kutoku tekeleza kikamilifu maazimio ya bunge huku wakitishia kuandamana nchi nzima endapo waliohusishwa na tuhuma za ufisadi wa Escrow hawatachukuliwa hatua za kisheria.
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha umoja huo ambapo amesema sheria ya maadili inatakiwa itungwe upya na utaratibu wa viongozi kutangaza mali zao uwe wa wawazi kwa wananchi na kuongeza kuwa maandamano hayo yana lengo la kulaani ufisadi wa Escrow pamoja na kushinikiza utekelezaji wa maazimio yote ya bunge.
 
Kwa upande wake katibu mkuu wa Chadema Dk Willbroad Silaa akizungumza katika kikao hicho amesema kuwajibika peke yake haitoshi badala yake hatua za kisheria zinatakiwa zichukuliwe ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimeonekana kujirudia mara kwa mara kutokana na watu kutenda makosa na kuishia kujiuzulu ili hali kuna hasara ambazo taifa limeingia.
 
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Mh James Mbatia ni miongoni mwa viongozi wa Ukawa walioshiriki kikao hicho ambapo ametumia fursa hiyo kuwasihi viongozi wa dini na viongozi wastaafu waliotumikia taifa kutumia siku kuu ya Noel kupaza sauti zao katika kuhakikisha serikali inasimamia haki na kwamba taifa lolote lenye migogoro haliwezi kupata ustawi wa jamii.

No comments:

Post a Comment