TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 26, 2014

JE, KWA HAYA BADO KUNA SERIKALI INAYOMILIKIWA NA WANANCHI, ILIYOTOKANA NA WANANCHI, KWA AJILI YA KUTIMIZA MATAKWA YA WANANCHI TANZANIA (DEMOCRACY)?.

JE, KWA HAYA BADO KUNA SERIKALI INAYOMILIKIWA NA WANANCHI, ILIYOTOKANA NA WANANCHI, KWA AJILI YA KUTIMIZA MATAKWA YA WANANCHI TANZANIA (DEMOCRACY)?.
(Ni ndefu lakini tumia muda wako kwa kutulia na kusoma)
Ndugu Watanzania wenzangu popote mlipo, nimshukuru mwenyezi Mungu aliyetupa uhai mpaka muda huu tunasherekea sikukuu ya Noeli na namuomba Mungu muweza atupe uhai tuuone mwaka mpya. Kwa wale waliotutoka kipindi chote cha mwaka au siku za mwisho kuelekea kuumaliza mwaka, Mungu aziweke roho zao mahala pema peponi. Amen...!
Nachukua fursa hii adhimu ya kuelekea mwisho wa mwaka kuakisi tulikotoka, kuangalia tulipo na kuchungulia (forecast) tuendako kama taifa la Tanzania na mustakbali wa nchi yetu.
Ukweli ni kuwa niwe mimi, wewe na yule hakuna sababu ya kunyamaza kama kuna jambo tunaweza kusema likaisaidia nchi kwa ajili ya kizazi chetu na kijacho. Najua kuna watu (wepesi wa kukata tamaa na kutotaka kuthubutu, wapendao business as ussual) wataniuliza "wangapi wamepita wakashindwa kuibadilisha nchi hii, wewe ndo uweze?". Ninachoamini ni kuwa wale wote wanaothubu kuongea kwa ajili ya ustawi wa taifa letu kuna waliotangulia walipanda mbegu ya mawazo hayo ndani yao, nao wasipofanikisha leo kuleta mabadiliko watoto wao wajukuu watayaleta kwa sababu ya msingi wa mabadiliko unaojengwa leo. Vinginevyo watoto na wajukuu wasingeyaleta kwa sababu wangeanza na msingi wenyewe.
Baada ya utangulizi huo bila kukuchosha, fuatana nami hatua kwa hatua kwa nilichokuandalia leo.
Kimsingi kukua au kutokua kwa nchi yoyote kiuchumi, kisiasa na kijamii kunategemea dira, sera na usimamizi wa serikali husika iliyopo madarakani.
Dira ni mwongozo wa taifa lolote ambayo kwayo, kila serikali inayoingia madarakani lazima itengeneze sera zitakazosaidia kufikia dira ya taifa. Dira ya taifa hulenga mipango ya muda mrefu kama taifa (kama miaka 50 na zaidi) ambayo kwayo hujipambanua kwa mataifa mengine. Mfano; enzi za Mwalimu, dira ya Tanzania ilikuwa ni kutengeneza jamii yenye ujamaa na usawa inayojitegemea (kiuchumi na kijamii) ndiyo maana katiba yetu ya 1977 ibara ya kwanza 3(1) inasema wazi kuwa Tanzania ni nchi ya kijamaa, isiyofungamana na dini yoyote na inayofuata demokrasia ya vyama vingi. Hili pekee linaipambanua Tanzania vilivyo.
Sera ni mipango ya serikali iliyopo madarakani (yenye dola) ambayo kwayo serikali iliyopo madarakani inatekeleza mipango ya kutekeleza dira ya taifa. Wakati wa Mwalimu alitengeneza sera ya vijij vya ujamaa ili watu wakae pamoja, wakizalisha na kugawana walichozalisha kwa umoja.
Kwa sasa, kila mwenye akili za kawaida anatambua kuwa taifa letu linaenda "bora liende" kama vile trekta lisilo na taa na dreva wake analala usingizi wa pono kwenye usukani. Najua tuna watu wazuri ndani yake ila "trekta” lilipopoteza mwelekeo linawapeleka msobemsobe.
Vyanzo vikuu vya hayo matatizo ni viwili.
1. Nchi kutokuwa na dira ya kufuata.
2. Kukosa viongozi wakuu bora ambao wapo tayari "ku-take risk" kwa lengo la "ku-reshape" nchi.
Wengi hawajui kuwa kama nchi sasa hatuna dira tunayofuata ili kuweka wigo njia kwa kila mwananchi kwa kila anachokifanya kilenge kutufikisha tunakotaka kama taifa. Tunajua sera ya Mwalimu ilikuwa ya ujamaa na kujitegemea na aliibaini hivyo kwenye katiba. Sera hiyo iliposhindwa, mambo yalianza kubadilika pole pole kuuelekea ubepari mpaka sasa ubepari umekomaa labda muda si mrefu tutaingia ubeberu, lakini viongozi wetu "kwa kumuogopa marehemu Mwali Nyerere" wameshindwa kuweka wazi kwenye katiba kuwa nchi yetu inafuata misingi ya kibepari. Athari ya kutoliweka wazi hili ni mvutano unaofanya tusinie mamoja kama taifa kuanzia kwa wananchi mmoja mmoja mpaka viongozi wetu. Hivyo wakati wengine wanapambana kuleta maendeleo kijamaa, wengine wanapambana kuleta maendeleo kibepari hivyo ni mgongano mkubwa. Ukitaka kuamini kuhusu hili, wafuate wabunge tofauti (rondom sampling) 5, waulize "Hivi Tanzania tunafuata sera gani? Ya ujamaa au ubepari? Majibu usinipe kwa sababu nayajua! Matokeo ya nchi kutokuwa na dira ya maendeleo ya nchi, inaanza kuongozwa kwa sera tu (mipango ya aliyshika dola kwa kipindi ambacho atakuwa madarakani). Akaja mtawala fulani akasema haoni umuhimu wa masomo ya sayansi katika kuendeleza taifa hili na badala yale tuwe na taifa la wacheza ngoma pekee, yanafutwa masomo ya sayansi na kubaki na masomo ya kucheza ngoma pekee mashuleni ili kuzalisha wacheza ngoma tu. Lakini nchi ingekuwa na dira, mfano: tunataka Tanzania iwe nchi ya kijamaa inayoendeshwa na uchumi wa viwanda (msingi wa maendeleo duniani kote) tungefanya "elimu hitajika" ndiyo nguzo pekee nchini. Siyo kilimo ni uti w mgongo, siasa ni kilimo wala kilimo kwanza kwa sababu nchi ikiwekeza katika elimu sahihi kwa watu wake ndipo maendeleo katika nyanja zote yanawezekana. Kinachobakia baada tu ya kuwapa elimu, ni kuwatengezea mazingira mazuri kila mwananchi mwenye ujuzi wa anachokijua kukifanya "precisely". Tukajifunze kwa Rwanda ( mhh..! Najua watawala hawaendi kuisikia kauli hii).
Shida kubwa ya pili tulionayo ni UONGOZI.
Taifa likifika lilipofikia hakuna tena kitakacholibadilisha mpaka mfumo wa viongozi wote waliopo watoke, waingie wengine ambao watakuwa tayari "ku-take highest risk ku-reshape" nchi. Si rahisi hata kidogo.
Umuhimu wa "ku-reshape" unatokana na;
1. Kukithiri kwa rushwa
Tumeshuhudi skendo za rushwa zinazovunja rekodi tangu nchi hii kupata. Shida ni kuwa rushwa hiyo inapita mpaka kwa wanaotakiwa kukemea rushwa, matokeo yake serikali nzima inamezwa mifukoni mwa mafisadi.
2. Kuzeeka kwa mawazo ya kiongozi.
Miaka 50 ni mingi sana kwa chaki kimoja kutawala nchi. Inafika wakati hakuwi mawazo mapya ya kuiongoza nchi ilihal ili uongozi uwe bora mawazo mapya na ubunifu vinahitajika. Kwa msingi huo, nawahakikishia Watanzani kuwa tungeanza kuonana maendeleo Tanzania kama upinzani ungechukua nchi 2015 kisha 2020 tena ichukue Ccm na baadaye kila anayeharibu angejua hachaguliwi tena. Matokeo yake ni maendeleo kwa wananchi.
3. Nepotism/ undugulism
Hili ni tatizo kubwa. Nenda kila sehemu, idara za serikali, vyombo vya dola kwenye vyama vya siasa nk utakuta zile krimu zote ni za vigogo wa serikali. Sisemi wao hawana uwezo na haki ya kufanya huko, laaah! Bali fuatilia CV zao na fanya ulinganifu na kipindi cha Nyerere. Inamaana nyerere watoto wake walikuwa mbumbumbu sana ukilinganisha leo ambapo mfano; baba mNEC, mama mNEC, mtoto mNEC, mkwe mNEC, shemeji mNEC, wakurugenzi wote BOT wenyewe, TISS wenyewe, nk.
4. Kushindwa kusimamia mipango yao na kila mtu kuwa na ya kwake serikalini.
Kuna suala la pembejeo na ununuzi wa mahindi napenda kulichukulia kama mfano wangu halisia wilayani kwetu Mbozi.
Kwanza serikali ilitangaza kununua mahindi wilayani Mbozi na kwingineko kwa kupima na kuyahifadhi ghalani huku ikizuia wafanyabiashara kupeleka mahindi nje ya nchi. Tangu serikali imepima mahindi hayo, wakulima/wafanyabiashara hawajalipwa pesa zao hadi leo. Kwa kweli watu sasa wanaamini shughuli ya kilimo ni biashara kichaa kwa sababu watu wapata mavuno na kupata neema ya soko zuri nje, mipaka huzuiwa kuwa serkali itayanunua na malipo yenyewe ndo huwa hivi. Mbons hatujasikia wafanyabiashara wa vinyago, nguo, cement nk wakipata soko zuri wakizuiliwa mipaka? Tunahisi kamfumo haka kamelenga kuwafanya wakulima watumwa wa kudumu kwa sababu hawana haki kabisa ya kupata bei nzuri ya mazao yao. Badala yake, mh. Godfrey Zambi aliwawezesha watu wake wa tatu wa karibu kisiasa ndiyo wakalipwa.
Zaidi ya hapo, naibu waziri wa kilimo na ushirika akijibu swali la Mh David Silinde mbunge wa Momba alimwambia mbolea ipo inakuja, lakini alipokuja mkurugenzi wa pembejeo alisema hazitakuwepo. Kwa sababu hiyo, tutegemee balaa la njaa mwakani.
For all those, lazima tuunganishe nguvu zetu kulinusuru taifa letu kwa kuiambia serikali ya CCM 2015 kapumzike uje tena kuomba 2020.
Nawatakia msimu mzuri wa sikukuu. Mungu awabariki.

No comments:

Post a Comment