TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 26, 2014

MLIPUAJI WA MABOMU SONGEA AJIKUTA AKILIPUKIWA YEYE NA KUPOTEZA MAISHA


Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akitoa
maelezo kwa DCP Diwani Athumani ambaye aliwasili mkoani humo jana
kwaajiri ya bomu la kutengenezwa kienyeji ambalo askari wa doria
walinusurika kurushiwa na kumlipukia mlipuaji wa bomu hilo ambaye
alifariki papo hapo.

Askari WP Mariam mwenye namba 8616 akiwa amelazwa wodi ya
majeruhi hospitali ya Mkoa baada ya kujeruhiwa mkono wa kushoto kwenye bega baada ya vipande vya bomu kumfikia akiwa na askari wenzake kwenye doria siku ya sikukuu ya krisimas.
  Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiuangalia mwili wa
mtuhumiwa wa ulipuaji wa bomu ambaye alitaka kuwarushua askari wa
doria wakati wa sikukuu ya krismas kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. (PICHA NA AMON MTEGA ,SONGEA)
-----------------------------------------

 NA AMON MTEGA,SONGEA
 
JESHI la Poilisi mkoani Ruvuma kwa kushirikiana na timu ya makachelo
toka makao makuu ya jeshi hilo wanawasakaka watu watatu ambao wanasadikiwa kujihusisha na ulipuaji wa mabomu huku mwenzao mmoja
akiwa amefia katika eneo la tukio baada ya kutaka kufanya jaribio la
kuwatupia  bomu askari waliyokuwepo doria katika sikukuu ya Krisimas ambalo lilimshinda na kumlipukia mwenyewe na kusababishakupoteza maisha papo hapo huku utumbo ukiwa umemwagika nje na  mkonowake wa  kushoto ukiwa umekatika kabisa na vipande vyake hajijulikanivilipo. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ukumbi wa mikutano wa
jeshi la polisi Mkoa wa Ruvuma Naibu Kamishna wa jeshi la Polisi,
kaimu mkurugenzi wa upelelezi wa Makosa ya Jina nchini (DCP)  Diwani
Athumani alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa 1.30
usiku huko katika mtaa wa Kotazi uliopo kata ya Majengo manispaa ya
Songea ,timu ya askari wakiwa doria kulitokea mlipuko wa kitu
kinachozaniwa kuwa ni bomu ambalo limetengenezwa kienyeji  nakusababisha kuwajeruhi  askari wawili .
DCP Athumani aliwataja askari waliojeruhiwa kuwa ni PC Mselem mwenye
namba G 7903 ambaye alijeruhiwa mkono wake wa kushoto na alitibiwa na kuruhusiwa na  mwingine PC Mariam mwenye namba WP. 8616 ambaye
amejeruhiwa kwenye bega la mkono wa kushoto na amelazwa katika hospitali ya Mkoa Songea(HOMSO)akiendelea kupata matibabu.
 Alisema kuwa timu ya makachelo toka makao makuu wakishirikiana na
tatu kwa mwaka huu. 
 
DCP Athumani alieleza zaidi kuwa wahalifu hao watakamatwa kirahisi
kutokana na tukio walilolifanya baada ya mwenzao kulipukiwa na bomu
hilo na kusababisha kifo chake walijaribu kutorosha mwili wa mwenzao
ili kupoteza ushahidi lakini ilishindikana baada ya askari polisi
doria wengine kuwahi eneo la tukio na wahalifu hao waliacha mwili wa
mwenzao na kutokomea kusikojulikana.
“Wahalifu hao waliuvuta mwili wa mwenzao kutoka katika eneo la tukio
kwa umbali wa mita zisizopungua 80 na 90 kwa lengo la kutaka kupotezausahidi  lakini waliwahiwa na askari wengine wa doria na kuuacha mwilina kutokomea kusikojulikana” alisema DCP Athumani.
Hata hivyo amewaomba wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini,wanasiasa,wazee, makundi mbalimbali  ya kijamii pamoja na
waandishi wa habari kuwa kitu kimoja katika kuwafichuwa waharifu hao
ili matukio hayo yasiweze kujirudia tena hususani Mkoa wa Ruvuma.
 Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu aliyetembelea
eneo la tukio na kuzungumza na waandishi wa habari kwa masikitiko
makubwa alisema kuwa waharifu hao wanaishi kwenye jamii inayotuzunguka hivyo ni vyema kila mmoja akaliona jambo hili kwa umuhimu wake wapekee kulipa uzito na kuwafichuwa wahalifu ili Mkoa uendelee kuwa naamani kwani linaleta taharuki kwa jamii jambo ambalo linarudisha nyumashughuli za maendeleo.
 Naye Mganga Mkuu mfawidhi Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma Dkt. Benedkto
Ngaiza amethibitisha kupokea mwili mmoja  wa mtu ambaye amekufa ukiwautumbo umetoka nje na  majeruhi wawili ambao ni askari na kwambaaskari mmoja alitibiwa jana na kuruhusiwa huku mmoja akiwa amelazwawodi ya majeruhi namba mbili  akiendelea kupatiwa matibabu na haliyake inaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment