TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 26, 2014

HOTUBA YA RAIS KIKWETE NA WAZEE WA DAR ES SALAAM - 12/22/2014

PESA ZA ESCROW SI ZA UMMA, ASEMA RAISI KIKWETE,
-ANADAI SERIKALI HAIKUPATA HASARA YOYOTE KUTOKANA NA SAKATA HILI,
-ATENGUA UTEUZI WA PROF TIBAIJUKA KWA KUKUBALI KUWEKEWA PESA KWENYE AKAUTI YAKE BINAFSI.
-AMUWEKA KIPORO PROF MUHONGO,WAKATI UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA,AKIPATA MAJIBU ATATOA UAMUZI.
-APANGUA BAADHI YA MAPENDEKEZO YA BUNGE.
-ADAI CCM WALIKUWA IMARA KWENYE SAKATA LA ESCROW
-AWATAKA CCM NAO WAKAWAAMBIE WANANCHI KUHUSU ESCROW
-AKIRI KUWA UJAMAA USHAKUFA KITAMBO
,huu ndi mchanganuo wa aliyoyasema rais  kikwete kuhusu ESCROW.
i) AMEKIRI KUWA TANESCO ILIKUWA INAIBIWA NA IPTL
ii) TRH 5.7.2006 NDIYO ACCOUNT YA TEGETA ILIFUNGULIWA NA KUFIKIA TAMATI TRH 5.9.2013 MAHAKAMA ILIAMURU SHUGHULI ZOTE ZA TANESCO ZIKABIDHIWE KWA IPTL HUKU KUKIWA HAKUNA KESI ILIYOFUNGULIWA ACHILIA MBALI ILE YA MWANZONI YA MALALAMIKO YA TANESCO KUWA WANAIBIWA KUPITIA CAPACITY CHARGE
iii). PESA ZILIKAAKWENYE ACCOUNT YA ESCROW KWA MIAKA 7.
iv) .Wakati CAG anakagua kulikuwa na shilingi 202 Bilioni nukta tisa.
v) Kama Tanesco wangeli tozo za uwekezaji,akaunti hii ingekuwa na shilingi Bilini 306.7,kutokana na Tanesco kutolipa ilibaki na madeniya shilingi Dola Bilioni 33.6 na IPTL.
vi) .Account ya Ecsrow haikuwa na Bilioni 306,bali zilikuwemo Bil 202 pekee ambazo IPTL ilikuwa inaidai Tanesco.
vii).Amesema kuwa kutoka na hali ya mgogoro ulivyokuwa pesa zilizokuwa ndani ya akaunti ya ESCROW SI ZA UMMA BALI NI ZA IPTL kwani ndiyo mlipwaji kutokana na madeni ambayo IPTL inaidai TANESCO kutokana na tozo za uwekezaji.
vii).Kuhusu majibu ya CAG,kuhusu pesa ni za nani?raisi amesema kama Tanesco wangeshinda mgogoro wao na IPTL basi pesa hizo zingekuwa za UMMA kama ilivyokuwa kwenye kesi yao ya mwaka 2001,ila kwa sababu Tanesco walishindwa,pesa hizi ni za IPTL na si UMMA(PUBLIC)
viii),KUHUSU KUWEMO KWA KODI ZA SERIKALI NDANI YA ESCROW ACCOUNT KIASI CHA BILIONI 21 NA MILIONI 700,AMESEMA PAP WALIPELEKEWA DENI LA KODI YA SERIKALI,AMESEMA CAG ALIKAGUA NA KUSEMA PESA ZILIZOKUWEMO KWENYE AKAUNTI YA ESCROW HAZIKUWA NA SIFA ZA KUITWA PESA ZA UMMA.
ix).Trh 15.9.2013 mahakama kuu ya Tanzania ulifanya uamuzi wa maombi ya kampuni ya VIP kuomba kusimamisha mchakato wa kuuza hiza za IPTL wakilumbana juu ya hisa,uamuzi wa mahakama ulikuwa PAP wapewe hisa 30 NA WAKANUNUA HISA 70 na waliandikisha hisa 70 Brela,mahakama ikaamua hisa zikabidhiwe PAP ambao ndiyo mmiliki halali wa IPTL.,Uamuzi huu wa mahakama ulimaanisha kuwa PAP wanatakiwa kumiliki mpaka pesa za ESCROW kwa PAP,umauzi ambao ulizuia malumbano serikalini juu ya akauniti ifungwe ama isifunwe,pesa zitoke ama zisitoke.
x).Wizara ya nishati na madini waliamu kuomba ushauri kwa mwanasheria mkuu juu ya pesa,AG alielekeza kuwa pesa zilipwe kama mahakama ilivyotaka,benki kuu waliuliza maswali haya,na AG akaelekeza walipe kwa PAP na hakuna kodi,ushsuri wa AG uliitoa nafasi ya akaunti kufungwa na kugawanywa rasmi na baadae kuingia barabarani.
xi).Maamuzi yote yaliyofanyika yalifanyika kwa maelekezo ya mwanasheria mkuu,umuzi huu wa mwansheria kuu umeibua mjadala mkuu kuwa kuna rushwa kubwa,watu wamemegewa mshiko,kila mtu kaongea.
xii).Amekanusha kuwa kufungwa kwa akaunti ya ESCROW hakukuwa na msukumo kutoka kwa maafisa wa serikali,amesema serikali ilifanya juhudi kubwa kwenye sakata hili.
xii).Amesema mwanasheria mkuu alimwambia hakukuwa na makosa yeyote kwenye maamuzi ya mahakama,na pia hakuna hasara ambayo serikali imepata kutokana na sakata hili la ECSROW kwa sababu pesa hizo zilikuwa ni deni ambalo Tanesco ilikuwa inadaiwa na IPTL.
xiii).Kuhusu kuwa PAP walinunua hisa za PIPAL LINK huku kikuwa na amri ya mahakama ya kutouza hisa,amesema bado vyombo vya mamlaka vinachunguza
xiv).Kuhusu uuzwaji wa hisa,amesema napo kunahitaji uchunguzi zaidi hasa bei ya hizi hisa.
xv).Amesema Rugemalira alilipa kodi aliyokuwa anadaiwa kiasi cha shilingi Bilioni 38,RUGEMALIRA hana makosa kwenye hili,Alilipa kodi zote.
xvi).KUHUSU MAPENDEKEZO CAG ameelekeza taaifa zile zipelekwe PCCB.
xvii).Kuhusu waliomegemewa pesa na RUGEMALIRA,amesema Takukuru na tume ya maadili ya watumishi wa umma wanachunguza na kushuhulika na watumishi wa umma wote waliopewa pesa,amesema tume ya maadili ya umma itawahoji wote waliopewa pesa.
KUHUSU MAZIMIO YA BUNGE
i.Amesema serikali imeyapokea maazimio na itayafanyia kazi
ii.Kuhusu kutaifisha mitambo ya IPTL,amesema si sawa kutaifisha sababu kutafukuza wawekezaji
iii.Kuhusu uwazi wa mikataba,amesema serikali itafanya mapitio ya mikataba,amesema kuna haja ya serikali na bunge kukaa pamoja na kuzungumza,kwa sababu kuna makampuni yanataka usiri wa mikataba(company secret)
iv)Kuhusu PCCB,na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vichukue hatua,amesema tayari utekelezaji ueanza.
v).Kuhusu kuwavua vyeo wenyevitio wa kamati amesema bunge ndilo litekeleza.
vi).Kuhusu kuundwa kwa tume ya kijaji kuwachunguza majaji waliohusika na sakata la ESCROW,amesema itabidi kuzingatia utaratibu wa kikatiba na sheria,amese suala hili linatakiwa kuanzia kwenye mahakama,halianzii kwa raisi wala bungeni,Amemuachia Jaji mkuu alishughulikie na kumpelekea mapendekezo raisi.
vii).Kuhusu mamlaka husika za kifedha na kiuchunguzi ziitaje Stanbic bank na benk zilizohusika zitangazwe kuwa taasisi zinazotakatisha fedha amesema uchunguzwe na mamlaka husika.
viii).Kuhusu serikali iandae na kuwasilisha marekebisho ya sheria ya uundwaji wa rushwa kubwa,amesema hilo ni wazo zuri,na serikaliimekuwa inaifanyia marekebisho taasisi ya kuzuia rushwa tangia mwaka 2008
ix).Kuhusu kuwavua nafasi zao watumishi wa umma wakiwemo mawaziri waliotajwa,raisi Kikwete amesema,Bodi ya Tanesco imeshamaliza muda wake,hili lishajifuta,kuhusu katibu mkuu Maswi amesema mamlaka zinazohusika zianze ushunguzi wa kuchunguza tuhuma zake,mwanasheria mkuu ameshajiuzulu,kuhusu mawaziri(TIBAIJUKA) amesema wamezungumza nae na wamekubaliana aachie ngazi,kuhusu Prof Muhongo amemuweka kiporo..

No comments:

Post a Comment