TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, December 23, 2014

CHADEMA chakosa maamuzi ya Jk kuhusu Escrow

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimekosoa maamuzi ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu kashfa ya ubadhilifu wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow kwa madai kuwa hatua alizochukua hazikuzingatia maazimio ya bunge.
Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Wilbrod Slaa
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Wilbrod Slaa amesema Rais Kikwete ameshindwa pia kutumia mamlaka ya kinidhamu aliyopewa na Katiba, kwa kushindwa kuwawajibisha watuhumiwa wa kashfa hiyo hasa majaji wanaotuhumiwa kuhusika katika sakata hilo.
Kwa mujibu wa Dkt. Slaa, hata utenguzi wa nafasi ya Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka haukufanyika kwa kuzingatia misingi ya utawala na kwamba hata kitendo cha kumweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo nacho kinaonesha jinsi serikali ilivyoshindwa kutekeleza maazimio ya bunge kuhusu hatua zinazostahili kuchukuliwa watuhumiwa wa Escrow.
Hivi karibuni Bunge la Tanzania lilipitisha maazimio nane ambapo miongoni mwa maazimio hayo ilikuwa ni pamoja na serikali kuwachukulia hatua za kinidhamu pamoja na kuwafuta kazi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika katika sakata hilo.

No comments:

Post a Comment