TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 26, 2014

FREDRICK SUMAYE: KUWENI NA HOFU YA MUNGU, NAYE ATASIKIA MAOMBI YENU KWA TAIFA

1Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama  Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sokoine tayari kwa tamasha la Krismas lililofanyika kwenye uwanja wa huo jijini Mbeya , Mh. Fredrick Sumaye amewaasa watanzania kumcha mungu na kuchagua viongozi waadilifu wenye uzalendo wa nchi, wenye kupenda na kuhurumia wananchi masikini na wenye hofu ya mungu ili kulinda amani ya nchi yetu jambo litakalofanya hata maombi  yanayofanyika  kuombea taifa la Tanzania yapokelewa  na Mungu, Tamasha hilo kesho linaendelea mkoani Iringa ambapo wakazi wa mjini Iringa wanapata nafasi nyingine ya kumcha mungu kwa njia ya uimbaji  2Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akisalimiana Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota kushoto ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama 3Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizindua albam ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya  yenye inayoitwa Mubhopege Pa Finganilo yenye nyimbo nane  kulia ni Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), David Mwasota na kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama. 4Katibu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Askofu David Mwasota akiiombea albam ya Mubhopege Pa Finganilo ya Kwaya ya Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali jijini Mbeya huku Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye,Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw Alex Msama na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakishiriki katika maombi hayo. 5Mwimbaji wa muziki wa injili Upendo Nkone akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati wa tamasha la Krismas leo. 6Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa jukwaani. 7Mwimbaji Ambwene Mwasongwe naye amesifu na kuabudu pamoja na mashabiki wake kama anavyoonekana akiwa akitunzwa na mashabiki wake wakati akiimba jukwaani. 10Tumaini Njole na wacheza shoo wake wakiwa angani wakati wakifanya vitu  vyao jukwaani.13
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akizungumza na mashabiki wa muziki wa injili. 21 
Edson Mwasabwite kulia ni Faraja Ntaboba kutoka DRC Congo wakionyesha vitu vikubwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. 23Mwimbaji kutoka Kenya Ritha Kisava ambaye ameshiriki Tamasha la Krismas kwa mara ya kwanza akiimba hii ilikuwa kama utabulisho wake kwa mashabiki wa muziki wa Injili nchini Tanzania. 25Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akiteta jambo na mmoja wa waratibu wa tamasha la Krismas Bw. John Melele wakati wa tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment