TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 24, 2014

Utamaduni Iringa wakaribisha Tamasha la Krismasi

image
Na Mwandishi Wetu
OFISA Utamaduni mkoa wa Iringa, Mwesiga Muhambo amelikaribisha Tamasha la Krismasi mkoani kwake kwa sababu ni siku ya kupokea zawadi duniani kote.
Kwa Mujibu wa Muhambo badala ya kusubiri kupokea zawadi wajitokeze kwenye Tamasha la Krismasi mkoani humo linalotarajia kufanyika Desemba 26 kwenye uwanja wa Samora.
“Zawadi yetu sisi wakazi wa Iringa ni Tamasha la Krismasi ambalo tunapata neno la Mungu kupitia waimbaji na viongozi mbalimbali wa dini,” alisema Muhambo.
Naye Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Athumani Haule alitumia fursa hiyo kuikaribisha Kampuni ya Msama Promotions mkoani humo kwa sababu ni fursa murua kwa wakazi wa mkoa huo.
Haule alisema anaamini kupitia Msama zitapatikana fursa mbalimbali na kuongeza chachu katika nyanja mbalimbali.
Katibu Mkuu wa CCM Iringa, Hassan Mtenga alitoa wito kwa wakazi wa Iringa kujnitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela.

No comments:

Post a Comment