TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 24, 2014

indexNa Mwandishi Wetu,

WAKATI Dunia ikisubiri saa kadhaa kabla ya sherehe ya Sikukuu ya Krismasi, Wakazi wa mkoa wa Mbeya na vitongoji vyake wamepewa wito na Umoja wa Kwaya ya makanisa mbalimbali mkoani Mbeya kujitokeza kwa wingi kwenye Tamasha la Krismasi linalofanyika (Desemba 25) leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini humo. Kwa Mujibu wa Mchungaji wa Kanisa la EAGT ambaye pia ni Mweka hazina wa Kwaya hiyo, Zacharia Mwakasaka kwaya hiyo inatarajia kushirikisha waimbaji zaidi ya 40 wa kwaya hiyo. Mchungaji Mwakasaka alisema wanakwaya hao kwenye mkesha wa sikukuu hiyo, Desemba 24 waliweka kambi ya siku moja kwenye chuo cha Uyole kwa lengo la kujiweka sawa kabla ya Tamasha hilo. Mwakasaka alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa Mbeya na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kushuhudia kwaya hiyo ambayo imekusanya madhehebu mbalimbali ya Kipentekoste ya jijini humo. Aidha Mwakasaka alisema Kwaya hiyo inatarajia kuzindua albamu yake ya Mubhopege Pa Finganilo yenye nyimbo nane nyimbo nyingine ni kama Ilisubha ‘Jua linachomoza’, Yesu alipokwenda, Jesu Bho Ikufyuka ‘Yesu alipopaa’, Matendo, Gwe Kyala Mwikemo ‘Mungu Mtakatifu’ na Nasobhile ‘Nilikuwa nimepotea msituni’. Mgeni rasmi mkoani Mbeya ni Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye.

No comments:

Post a Comment