TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 27, 2014

RUSHWA YATAWALA CCM- LOWASA AMWAGA MAMILIONI ZANZIBAR NA TANZANIA BARA KUSAKA URAIS

Naomba kuwauliza CCM kuipitia kamati ya maadili inayoongozwa na mzee wangu Philip Mangula, haya yanayofanywa na Edward Lowassa na Genge lake ya kumwaga mamilioni huko Unguja, Pemba na Tanzania bara kwa
wajumbe wa NEC na mkutano mkuu hamyajui au mmeyabariki?
Naomba kuiuliza EL ni nani mpaka akidharau chama namna hii? mamilioni haya yanayogaiwa hadharani kuanzia huko Unguja na Pemba kuelekea nchi nzima hamyaoni? Tena yakiwahusisha baadhi ya mawaziri wa SMZ na Jamuhuri ya Muungano?
Tangu juzi, kundi la wapambe wa Edward Lowassa na yeye mwenyewe wakiwa Zanzibar, wamekuwa wakigawa shilingi 1,000,000/= kwa kila mjumbe wa NEC CCM, na shilingi 500,000/= kwa kila mjumbe wa mkutano mkuu.
UNGUJA
Rushwa ya huku ilikuwa ikiratibiwa na kusambazwa na wana CCM wafuatao:-

-Jamali Juma (naibu katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar zamani)
-Omar Yusuf Mzee (waziri wa serikali ya SMZ)
-Masauni Masauni (mbunge JMT)
-Machano Othman Machano (naibu waziri SMZ)
-Haji Omar Kheri

PEMBA:
Fuko la rushwa la Pemba lililoanza kugawiwa jana linaratibiwa na wafuatao:-

-Makongoro Mahanga (naibu waziri wa kazi JMT)
-Mwenyekiti wa CCM (w) Ilala
-Muhammed Abdulaziz (mkuu wa mkoa mstaafu)

Hivi sasa wagawaji wa rushwa wako wilaya ya MKOANI huko Pemba.
Tunakwenda wapi?
Kamati ya maadili CCM iko wapi?
Lowassa wajumbe wa NEC wako zaidi ya 200, wajumbe wa mkutano mkuu wako zaidi ya 3000, pesa hizi wewe na genge lako mtazirudishaje mkiingia Ikulu?
Watumishi wa Mungu mko wapi? Genge hili linatuvurugia nchi?
Philip Mangula uko wapi?
Tanzania nakupenda.

No comments:

Post a Comment