TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 25, 2014

Nyumba zaidi ya 51 zimebomolewa na mvua na kusababisha wakazi zaidi ya 200 kukosa makazi Singida.


Na:

Zaidi ya nyumba hamsini na moja zinazokadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya miambili katika manispaa ya Singida zimebomolewa na mapaa yake kuezuliwa na mvua kubwa iliyonyesha ya mawe ikiwa na upepo mkali iliyo dumu kwa dakika ishirini.
Mvua hiyo ambayo ilianza kunyesha majira ya saa kumina mbili jioni siku ya tarehe ishirini na tatu imesababisha hasara kubwa kwa wakazi wa manispaa ya Singida, jitihada za kumpata mkuu wa wilaya ya Singida Bi Queen Mlozi ili kuelezea tukio hili zimepatikana na kueleza kuwa mpaka sasa nyumba hamsini na moja zimeharibiwa ikiwemo nyumba za watu binafsi na madarasa ya msikiti na kusema kuwa serekali imejipanga kuwasaidia watu walio athirika. 
Akieleze diwani wa kata ya mitunduruni Bwana Pantaleo Sorongai amesema mvua iliyonyesha imeleta madhara makubwa na ameomba serekali kutoa msaada wa mahema na chakula kwa wakazi ambao wameathirika kwani hawana sehemu za kujisitiri. 
Kwa upande wao wakazi wa manispaa ya Singida wamesema mvua iliyo nyesha haija wahi kutokea  pamoja na kunyesha muda mfupi imeleta madhara makubwa na wamelalamikia manispaa ya Singida kwa kutokutengeneza vizuri miundombinu ya maji na kusababisha nyumba nyingi kubomoka.

No comments:

Post a Comment