TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 24, 2014

Vijiji 45 mkoani Mara kupatiwa umeme

indexaWaziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa vijiji vipatavyo 45 vilivyopo katika mkoa wa Mara vinatarajiwa kuunganishiwa na huduma ya umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Profesa Muhongo aliyasema hayo katika ziara yake ya siku sita katika mkoa wa Mara lengo likiwa ni kukagua na kuzindua miradi ya umeme vijijini inayosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Profesa Muhongo alisema ziara yake iliyohusisha wilaya za Musoma Vijijini, Tarime, Rorya, Bunda na Serengeti ililenga pia kubaini na kukagua mahitaji ya umeme katika wilaya hizo ili vijiji vilivyokosa umeme kwenye awamu ya pili viingizwe katika awamu nyingine ya umeme vijijini. Alieleza kuwa Wizara imekuwa ikisambaza umeme katika kila Mkoa na Wilaya za Tanzania kwa awamu kulingana na mahitaji na idadi ya watu katika maeneo hayo. Alisema kwa sasa umeme unaosambazwa upo katika awamu ya pili ambapo awamu ya tatu itakuja baada awamu ya pili kumalizika. Alisema vipaumbele vinavyotolewa katika uunganishaji wa umeme vijijini Profesa Muhongo alitaja kuwa ni maeneo yenye huduma muhimu za kijamii kama vile mashule, vituo vya afya, makanisa, misikiti, ofisi za vijiji na kata, na sehemu zenye miradi ya maji. “Lengo letu kuu kwanza ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za jamii kwa urahisi na baada ya kuboreshwa kwa huduma hizo tunakwenda kuwaunganishia umeme wananchi mmoja mmoja, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha maisha ya wananchi yanaboreshwa kupitia nishati ya umeme”, alisema Profesa Muhongo Profesa Muhongo aliongeza kuwa ili nchi yoyote duniani iweze kupiga hatua katika ukuaji wa uchumi wake, inahitaji nishati ya umeme na kuongeza kuwa kwa kutambua hilo serikali imeanza kwa upande wa vijijini ili wananchi hao waweze kujiingizia kipato kupitia ajira za kujiajiri. Alifafanua kuwa wananchi wa vijijini kupitia nishati ya umeme wanaweza kuwekeza kupitia mashine za kusaga nafaka, kukamua mafuta, kuhifadhi vyakula vya kuuza kwenye majokofu na kujipatia fedha na kuongeza kuwa itapunguza wimbi la watu kukimbilia mjini kutafuta ajira Wakati huohuo Mwenyekiti wa kijiji cha Bukabwa Thomas Makwera alisema kuwa wananchi wa kijiji chake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kutokuunganishiwa umeme kwa muda mrefu hali inayopelekea maendeleo ya kijiji hicho kudorora. Hata hivyo aliongeza kuwa wakandarasi wamekuwa wakionekana wakisimika nguzo za umeme hali inayotia hamasa kwa wananchi ya kutaka kujua ni lini wataunganishiwa na huduma ya umeme. Akijibu swali la Mwenyekiti huyo Profesa Muhongo alimtaka mkandarasi anayesimamia mradi huo kutoka kampuni ya Derm Electrical Huseni Ayubu kutoa ufafanuzi ambapo mkandarasi huyo alieleza kuwa kazi ya kusimika nguzo pamoja na kuunganisha umeme inatarajiwa kukamilika mapema Februari mwakani. Naye Profesa Muhongo aliwataka wanakijiji wa Bukabwa kuchangamkia fursa ya kuunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 27,000. wakati mradi wa umeme ukiwa bado upo katika kijiji chao. Alisema kuwa lengo la utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote ambavyo umeme umepita lakini havijaunganishiwa vinaunganishiwa ili kuhakikisha vijiji vyote vilivyopitiwa umeme vinapata umeme kwa kufuata utaratibu huo.

No comments:

Post a Comment