TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 24, 2014

Profesa Anna Tibaijuka “Bwana alitoa na Bwana ametwaa.” ni baada ya kufukuzwa uwaziri


Siku moja baada ya kufukuzwa  uwaziri, Mbunge wa Muleba Kusini (CCM),  Profesa Anna Tibaijuka amewasili jimboni kwake na kusema, “Bwana alitoa na Bwana ametwaa.”
Profesa Tibaijuka alivuliwa uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Rais Jakaya Kikwete juzi kutokana na kuhusika kupokea fedha katika akaunti binafsi.
Baada ya kuwasili na kupokewa kwa maandamano, Profesa Tibaijuka aliwaomba wananchi kukaa kimya kwa dakika moja ili kumkumbuka katibu wake wa jimbo aliyefariki dunia wakati sakata hilo likijadiliwa bungeni.
Profesa Tibaijuka aliyepokewa kwa msafara wa magari kutoka Uwanja wa Ndege wa Bukoba, aliwaeleza wananchi kuwa ilikuwa ni lazima kutafuta msaada kwa watu wengi ili aweze kuwasomesha watoto anaowasaidia kielimu.
“Kuna suala la escrow, zamani kulikuwa na aspro ambayo ilikuwa ni dawa ya kweli, sasa suala hili limefikia tamati hamkunichagua ili nikawe waziri, ni sawa na kusema Bwana alitoa na Bwana ametwaa,” alisema Profesa Tibaijuka.
Aliambatana na mtoto wa kike akisema ni mmoja wapo wa wanafunzi wasio na uwezo anaowasomesha katika Shule ya Babro Johanson, inayotajwa kuwa ndiyo iliyopokea Sh1.6 bilioni alizoingiziwa katika akaunti yake binafsi, katika Benki ya Mkombozi.
Profesa Tibaijuka alitumia muda mfupi kuelezea suala la kuhusishwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow akisema Taifa lina changamoto ya kupata elimu bora na wapo viongozi wachache kama yeye wenye moyo wa kusaidia masuala ya elimu.
“Teknolojia sasa imekua, naamini mlikuwa mnafuatilia mambo yalivyokuwa yanakwenda, yalikuwa ni mambo makubwa, kazi ya uwaziri nisingeipata bila nyinyi wananchi. Nilikuwa na majukumu mengi, sasa nitapata muda wa kukaa jimboni.
“Taifa bado lina changamoto ya kupata elimu bora, hiyo shule mnayoisikia ada yake kwa mwaka ni zaidi ya Sh4 milioni, hivyo lazima nitafute mtu wa kunisaidia. Hakuna mtoto  wangu hata mmoja anayesoma kwenye shule hizo,” alisema Tibaijuka.
Huku hotuba yake ikikatizwa na watu waliokuwa wakishangilia, Profesa Tibaijuka aliwaonya wanaotaka kulinyemelea jimbo hilo kuwa yuko ‘fiti’ na anawasubiri kukutana nao ulingoni.
Alisema atakuwa tayari kufanya kazi katika maeneo yanayoongozwa na vyama vya upinzani jimboni kwake akiamini kuwa pia wapo wanachama wa CCM.
>>>Mwananchi

No comments:

Post a Comment