TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, December 26, 2014

PATCHO MWAMBA AKANUSHA KUFUMANIWA, KUPIGWA

Patcho Mwamba akiwa katika ofisi za Global Publishers Ltd leo.
Picha ya Patcho iliyozua utata mitandaoni.
MWIGIZAJI na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba hivi punde ameibuka katika ofisi za mtandao huu na kukanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.
Akiongea na Full Utamu, Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni aliipost mwenyewe juzi baada ya kupata aleji ya macho kwa lengo la kutafuta uumbuzi wa kupata dawa kwa watu watakaokuwa na dawa za hilo tatizo na kwamba baada ya kufanya hivyo ametokea Mtu mmoja akumtaja jina ambaye ni Mdada aliyeiweka kwenye mitandao baada ya kukurupuka bila kusoma maelezo aliyokuwa ameyasema katika kuomba msaada huo kwa watu wanaofahamu dawa za aleji ya namna hiyo.
Mdada huyo ambaye kwa namna ingine patcho anasema imemshangaza sana kutokana na kuweka habari ambazo zilikuwa hazina ukweli wowote. ambapo baadaye ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi.
"Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe
juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho akiwa katika ofisi za mtandao huu zilizopo Mwenge-Bamaga, Dar.

No comments:

Post a Comment