TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 25, 2014

Usiku wa Black &White 55th Birthday Bash ya Asia Idarous Khamsin wafana

DSC_0018
NA: ANDREW CHALE.

SHEREHE maalum ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 55 ya kuzaliwa kwa Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin ‘Black &White 55th  Birthday Bash’   usiku  wa Desemba 24 ulifana  huku Spice Modern Taarab  wakikonga nyoyo wadau mbalimbali waliojitokeza ndani ya M.O.G Bar (Zamani Nyumbani Lounge) katika tafrija hiyo.
Sherehe hizo zilizoandaliwa na  Wabunifu wa mavazi wachanga na  wanaochipukia nchini,  uliojulikana kama ‘Black &White 55th Birthday Bash  Asia Idarous Khamsin’  ambapo wadau mbalimbali walipata wasaha wa kujumuika pamoja sambamba na burudani hiyo ya  Spice Modern taarab.
Kwa upande wake, Asia Idarous Khamsin  alimshukuru Mungu kwa mema anayomtendea hadi kufikisha miaka 55, ambapo aliitaka jamii kuendelea kusimamia mema ikiwemo matendo yampendezayo Mwenyezi Mungu.
Aidha, wadau mbalimbali walijitokeza kwenye tafrija hiyo, wakiwemo wabunifu, wasanii na watu maarufu. Wakiwemo wabunifu Rio Paul, Martin Kadinda, Faustian Simon na wengine wengi ambao wanachipukia kwa sasa kwenye tasnia hiyo.

No comments:

Post a Comment