TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, December 22, 2014

RIDHIWAN AKITEMBELEA SHULE YA MSINGI CHANGALIKWA NA KUJIONEA CHANGAMOTO ZINAOIKABILI

unnamedMbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, wa kwanza kulia alipotembelea ujenzi wa vyoo vya kisasa vinavyojengwa katika shule ya msingi Changalikwa,wa pili kushoto mwalimu mkuu wa shule hiyo Juma Paulo na wa kwanza kushoto ni mwalimu mkuu shule ya sekondari Lugoba Abdalaah Sakasa.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
………………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
WANAFUNZI wa shule ya msingi ya Changalikwa ,kata ya Mbwewe,chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wanatarajia kuondokana na kero ya vyoo chakavu na kujisaidia maporini baada ya halmashauri ya wilaya hiyo kuanza ujenzi wa matundu 6 ya vyoo .
Ujenzi huo umelengwa kugharimu kiasi cha sh.mil 10 zilizotolewa kupitia fedha za mradi wa usafi na mazingira huku ukitarajiwa kukamilika baada ya miezi miwili ijayo.
Vyoo hivyo vitakapokamilika kutawezesha wanafunzi wa shule hiyo kuondokana na adha ya kwenda kujisaidia maporini kama ilivyo kwasasa.
Akizungumzia ujenzi wa vyoo hivyo juzi wakati mbunge wa jimbo hilo Ridhiwani kikwete alipokwenda kutembelea ujenzi huo,mwalimu mkuu wa shule ya msingi changalikwa Juma Paulo amesema kuwa vyoo vya awali vimechakaa miundombinu yake hivyo haifai kwasasa kutumiwa na wanafunzi kwa kuhofia kudondokewa na kuta ama madahara mengine.
Aidha Paulo amesema, kutokana na uchakavu uliokithiri wa vyoo hivyo, baadhi ya wanafunzi walikua wakilazimika kujisaidia porini hali ambayo inaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Nae mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete aliyetembelea ujenzi huo alieleza kuwa shule hiyo ilipata msaada huo kutokana vikao mbalimbali vya halmashauri kutambua tatizo lililopo ili kuwajengea wanafunzi mazingira bora.
Amesema kijumla tatizo la vyoo mashuleni si zuri kwa afya za wanafunzi sanjali na walimu kwani linatishia afya za binadamu hivyo haina budi kutatua hali ya uchakavu wa vyoo uliopo katika shule hiyo.
Ridhiwani ameeleza kuwa yeye kama mbunge atasaidia kuweka tanki la kuhifadhia maji ambalo litatumika kuvuna maji kwa ajili ya wanafunzi na walimu wa shule hiyo ya msingi Changalikwa..
Shule ya msingi Changalikwa ina jumla ya wanafunzi 405,walimu 6.

No comments:

Post a Comment