
…………………………………………………………………………..
Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze
Wazee wa kijiji cha Msoga,katika
kata ya Msoga ,Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ,wamemkabidhi
zana za jadi mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ikiwa ni moja
ya ishara ya kumpokea kijijini hapo rasmi..
Wazee hao walifanya shughuli hiyo mapema juzi na kumtaka mbunge huyo kuendelea umoja na mshikamano nadani ya jimbo hilo.
Nae Ridhiwani Kikwete
akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zana hizo amewashukuru wazee hao
na kuahidi kutekeleza masuala ya maendeleo ili jimbo hilo liweze kutoka
katika hatua iliyopo sasa.
Aidha Ridhiwani amesema suala la
mila na desturi linatakiwa lidumishwe pasipo kulipa kisogo kwa faida ya
vizazi vya sasa na baadae .
No comments:
Post a Comment