TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, December 21, 2014

KITUO CHA RADIO 5 WAFANYA KAMPENI YA USHINDI KWA WATOTO YATIMA

SAM_0388
Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 Arusha wakikabidhi misaada mbalimbali katika kampeni ya “USHINDI”inayoendeshwa na kituo hicho,misaada hiyo ilitolewa na wahisani mbalimbali kwaajili ya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima Mkoani Arusha,katika Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo kushoto ni Sarah Keiya wakiwakabidhi watoto wa kituo cha kiwohede ndoo ya mafuta ya kupikia kwaajili ya sikukuya Krismass na mwaka mpya jijini hapa jana katika hotel ya world Garden
SAM_0393
Wafanyakazi wa kituo cha redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo cha kiwohede na huruma katika hotel ya world Garden iliyopo moshono jijini Arusha katika tam
SAM_0390
Mkuu wa vipindi wa kituo hicho Mathew Philip akikabidhi moja ya msaada kwa shcha watoto huruma
SAM_0363
Watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima wakishindana kucheza muziki
SAM_0376
Grace Joseph(12)wa kituo cha Kiwohede akionyesha ujuzi wake wa kucheza katika shindano
SAM_0400
Mtoto anayeishi katika mazingira magumu akiwa jukwaani akiimba wimbo wa “NISEME”wimbo wa Ya moto band
SAM_0358
Mashindano yakiwa yanaendelea
SAM_0361
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa mzigoni
SAM_0385
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba moja katika shindano la kucheza muziki
SAM_0384
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe mshindi namba mbili baada ya kushinda katika shindano la kucheza muziki
SAM_0364
SAM_0346
Wafanyakazi wa redio5 wakiwa wanaanda sausage kwaajili ya watoto yatima
SAM_0352
Muonekano wa watoto wakiwa katika eneo la kuchezea michezo mbalimbali
SAM_0350
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Bi.Vicky Mwakoyo akiwa na  Meneja masoko wa Redio 5Bi.Sarah Keiya
SAM_0366
Mtangazaji wa kituo hicho Akiba Kilango ambaye alikuwa MC wa shughuli hiyo akiwa anaongea na watoto jukwaani kabla ya mashindano ya kucheza kuanza
SAM_0371
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anafatilia tamasha hilo
Kampuni Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina “Kampeni ya USHINDI”linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Arusha
Mkurugenzi wa kituo hicho  Robert Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao wasijione kutengwa
Meneja  ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao ni wale wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na tukifanya hivi watajiskia vizuri
Meneja masoko wa Redio 5 Sarah Keiya ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio 5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful company,World garden.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

No comments:

Post a Comment