Moja
kati ya studio ambayo inafanya vizuri katika utayarishaji wa muziki
jijini dar es salaam sinza lego Flexible music imekuja tena na Mfalme wa
Rhymes Afande Sele na ngoma yake mpya inayoitwa Mwendo kasi aliyoifanya
katika studio hizo.
Mwendo
kasi ni ngoma ambayo inaelezea ajali mbali mbali zinazotokea barabarani
ambazo zinasababishwa na uzembe wa madereva na kusababisha vifo vya
wananchi, akiwa amewashrikisha wasanii kutoka mkoani Morogoro Dyna
Nyange na Ballet.
Pia
wimbo huo ambao umetengenezwa na mtayarishaji kutoka Flexible Music
anayeitwa Mbatizaji akiwa ameutengeneza kwa kiwango cha hali ya juu
kutokana na vyombo na ubora wa studio, hata hivyo katika wimbo huo ambao
umefafanua mambo mengi yatokeayo barabarani.
Kwa
mashabiki wa Afande Sele mkae tayari kwa kile kitu ambacho amekizungumza
katika wimbo huo maana amezungumza mengi kama unavyojua Mfalme wa
Rhymes huwa akitoa kitu hakosei kwa mashabiki wake.
Katika
wimbo huo amewazungumzia kwa wale madereva ambao wanakunywa pombe kisha
wanaingia barabarani kumata uskani na kuendesha gari kwa mwendo wa kasi
na kusababisha ajali pia ameongea kuhusu abiria ambao wanakaa kimya
wakati dereva akiwa anaendesha gari kwa kasi.
Na
Pia kwa madereva ambao wanaongea na simu huku wanaendesha magari, pia ku
overtake katika kona kali maana nao wanaweza kusababisha ajali na
kupoteza uhai wa binadamu maana uhai hauji mara mbili.
No comments:
Post a Comment