Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
MABINGWA
wa soka Tanzania bara na wawakilishi pekee wa nchi katika mashindano ya
kimataifa, klabu ya Yanga ya Dar es salaam imeanza kujifua jana
kuelekea katika mechi ya marudiano dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi ya
mabingwa barani Afrika, klabu ya National Al Ahly ya Misri itakayopigwa
mjini Cairo jumapili machi 9 mwaka huu.
Yanga
wataingia uwanjani wakiwa na mtaji wa ushindi wa bao 1-0 walioupata
katika mchezo wa awali, uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam machi mosi
mwaka huu.
Bao hilo pekee lilifungwa dakika ya 82 kupitia kwa nahodha na beki wake wa kati Nadir Haroub `Canavaro`.
Kuelekea
katika mchezo huo, kiungo wa zamani na nahodha wa Yanga, Ali Mayay
Tembele amewashauri wana Jangwani kujiandaa vizuri kwani Waarabu
wataingia kwa nguvu kubwa kuhitaji kufuta matokeo ya mchezo wa awali.
No comments:
Post a Comment